Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

2014 Ulikuwa mwaka wa Taylor Swift.

maxresdefault
 Mwaka wa 2014 ulikuwa mwaka mzuri kwa nyota wa Muziki wa Pop Taylor Swift baada ya mwanamuziki huyo kumaliza akiwa ameongoza kwenye orodha ya wasanii waliouza albamu nyingi nchini Marekani .
Kwa mujibu wa kampuni ya Nielsen Music , Albamu ya 1989 iliyotolewa na Swift mwneye umri wa miaka 25 iliuza jumla ya nakala milioni 3.6 idadi ambayo ilikuwa kubwa kwa kopi za albamu zote kwa mwaka 2014.
Albamu ya the Frozen ambayo nyimbo zake zilitumika kwenye movie ya The Crown ilifuatia kwa mauzo ikiwa imeuza nakala milioni 3.53.
Cha ajabu ni kwamba albamu hii ya The Crown iliongoza kwa mauzio kwa kipindi cha miezi 12 kabla ya kupitwa kwenye mauzo kati wiki za mwisho za mwezi desemba ambapo ilipitwa na albamu ya Taylor Swift baada ya albamu hiyo ya 1989 kuuza kopi 326,000 katika kipindi cha wiki moja.
Albamu ya The Crown iliyotumika kwenye movie ya Frozen ilishika nafasi ya pili.
Albamu ya The Crown iliyotumika kwenye movie ya Frozen ilishika nafasi ya pili.
Alabmu hizi mbili ndio albamu pekee zilizofanikiwa kuuza kopi milioni 3 kwa kipindi cha mwaka 2014 .
Albamu ya tatu ilikuwa albamu ya Sam Smith iliyoitwa The Lonely Hour ambayo iliuza kopi milioni 1.21 ikifuatiwa na albamu za Beyonce , Lorde na One Direction pamoja na albamu ya mwanamuziki mkongwe Barbara Streisand
Disney Music Group ambao walisimamia albamu ambazo zimetumika kama soundtrack kwenye movie za Frozen na Guardians of The Galaxy wamefanikiwa kuingiza albamu mbili kwenye albamu tano bora kwa mara ya kwanza kwenye historia ya takwimu za Nielsen Music .
Hii ni mara ya pili kwa Taylor Swift kumaliza mwaka akiwa na albamu bora kimauzo kwa Marekani baada ya albamu yake ya mwaka 2009 ya Fearless kumaliza ikiwa juu baada ya kuuza kopi milioni 3.22
 Albamu ya Beyonce iliingia kwenye top 10 ya albamu zilizouza nakala nyingi kwa mwaka 2014.

Albamu ya Beyonce iliingia kwenye top 10 ya albamu zilizouza nakala nyingi kwa mwaka 2014.
Chati Rasmi ya Albamu Za Marekani kwa Mwaka 2014
1.Taylor Swift – ‘1989’
2.Disney Music Group – ‘Frozen’ soundtrack
3.Sam Smith – ‘In the Lonely Hour’
4.Pentatonix – ‘That’s Christmas To Me’
5.Disney’s Hollywood Records – ‘Guardians of the Galaxy’ soundtrack
6.BeyoncĂ© – ‘BeyoncĂ©’
7.Barbra Streisand – ‘Partners’
8.Lorde – ‘Pure Heroine’
9.One Direction – ‘Four’
10.Eric Church – ‘The Outsiders’
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top