
Utata umeibuka baada ya sister wa Kanisa Katoliki huko Italy aliyekuwa
akilalamikia maumivu ya tumbo na kukimbizwa Hospitali na kujifungua
mtoto wa kiume licha ya kuishi katika Jumuiya hiyo ya wanawake watupu.
Sister huyo mwenye umri wa miaka 31 yupo kwenye kikundi cha masista cha
Santa Chiara Italy, asili yake ni Amerika ya Kusini, alilalamikia
maumivu makali ya tumbo baadaye alianguka, madaktari walifika katika
eneo hilo na baada ya kumfikisha Labour alijifungua.
Watu wengi wameshindwa kuelewa kwa jinsi gani ameweza kupata ujauzito licha ya kula kiapo cha usafi wa moyo na utii.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment