*Tafiti Mpya Za Kitaalamu Zadhihirisha Uhalali wake Kisiasa
*Kauli ya Jk yaongezewa nguvu na Tafiti Mpya za PTT
*Kauli ya mjumbe kamati kuu Jerry Slaa Yampa majibu nape na January
"Chama chetu lazima kipeleke bidhaa inayohitajika sokoni, inayouzika na
inayokidhi haja ya mnunuaji"
*Tafiti zabainisha nguvu ya Wapinzani Wa Lowassa Pinda na Membe,
washindwa kutumia System kumzima Lowassa Zaweka wazi ushawishi wa
Lowassa Kwa Umma.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Positive Thinkers Tanzania imetoa ripoti
yake ya utafiti kuhusu mwanasiasa anayekubalika zaidi na wananchi katika
nafasi ya Rais ajaye, Lowassa aongoza na nafasi ya 2 imeenda kwa Dr.
Wilbroad Slaa huku Mwigulu Nchemba aking'ara kama kijana aliyeongoza kwa
kukubalika kwa kukamata namba 3.
Ifuatayo ni orodha ya wanasiasa waliongia 10 bora na asilimia ya kura walizopata.
1. Edward Lowassa 22.8%
2. Wilbroad Slaa 19.5%
3. Mwigulu Nchemba 10.6%
4. Ibrahim Lipumba 8.9%
5. John Magufuli 6.8
6. Zitto Kabwe 6.7 %
7. Bernard Membe 5.9%
8. Mizengo Pinda 3.2%
9. January Makamba 1.6%
10. Mark Mwandosya 1.2%
Tafiti hizi zimedhirisha nguvu na ushawishi aliyonayo Edward Ngoyayi
Lowassa Kama Kiongozi Kwa Jamii na Umma Wa Tanzania kwa Kiwango Cha
Asilimia Alichopata Lowassa Ni dhahiri Shahiri Uchaguzi Ukifanyika leo
basi ana nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo.
Hii ni Tofauti na Wagombea wengine ndani ya CCM ambao kama watapitishwa
na chama, chama kitalazimika kutumia nguvu kubwa mno ili kupata ushindi
na ushindi ambao unaweza ukawa wa asilimia moja tena baada ya uchaguzi
kurudiwa ikiwa ni sehemu ya marudio baada ya round ya kwanza kuonekana
kutofikia asilimia.
Tafiti hizi zinaipa kauli ya Mh mwenyekiti na Rais wa tanzania Amiri
jeshi mkuu nguvu kwani alisema " ikitokea kuna mtu ananguvu ya kutosha
na mnamuona anafaa kuwa Rais basi msisite kumshauri agombee, eeh
mshawishini tuuh" kwa muda wa week sasa makundi mbali mbali kada na rika
mbali mbali kutoka katika kila kona ya tanzania yamekuwa yakijitokeza
kwenda kumuomba Lowassa agombee urais.
Kwa Tafiti hizi watu watapata majibu ni nani anafaa na kwa nini mamia ya
watanzania wanajitokeza kumshawishi Edward Lowassa Agombee,Alisema hivi
karibuni mjumbe wa kamati kuu ndugu jerry silaaa Yakwamba " chama
lazima kipeleke mgombea anayekubalika anayeuzika na anayeweza kukipa
chama ushindi" kauli hii ilikuwa mwiba na jibu kwa nape aliyewahi kutoa
kauli isiyo ya kiungwana kwa kusema chama hakiwezi kumpitisha mgombea
asiyesafishika hata kwa dodoki.
Kauli hii inapingwa na takwimu za tafiti za kitaalamu kwamba Lowassa Ni
sawa na kiatu kilichokwisha pakwa kiwi ni kazi ya chama kukibrush tuu"
pia kauli hii ni jibu linalomjibu January makamba yakwamba Lowassa
Alishapita umri wa kufanya siasa ya maigizo tafiti hizi zinaonyesha
namna january anatakiwa kukuza siasa yake watanzania Wamfahamu zaidi na
apate uhalali wa kisiasa.
Alisema mama Sophia simba mjumbe wa kamati kuu Kumjibu januaru " kama
unaona wenzio wanaigiza kwa kutoa pesa ili watu wawashawishi nawe toa
pesa tuone kama kuna mtu atakuja kukushawishi"Pamoja na nguvu kubwa ya
kibobezi inayotumiwa na wabobezi hawa wawili pinada na membe bado siasa
yao imeonekana kukosa uhalali kwa watanzania tafiti za za kitaalamu mara
kwa mara zimekuwa sio rafiki kwa pinda na membe kwa takwimu za tafiti
kwa chama cha ccm kumpitisha membe au pinda ni sawa na kupeleka KOFIA YA
POLICE DUKANI UKAIUZE Nguvu ya Mwigulu Lamerck Nchemba Imeonekana kuwa
Kubwa Kuliko Hata Wabobezi hawa wawili wanaotumia ubobezi wao kupitia
system ya serekali na dola kushinikiza makundi mbali mbali kuwaunga
mkono.
Hivi karibuni kumekuwa na tabiya ya makundi mbali mbali yanayopewa na
kupokea vitisho kutoka kwa wabobezi hawa wawili kwa kosa la kutumia
uhuru wao na Dhamira yao njema ya kumshawishi edward atangaze nia na
agombee urais.
UKIUWA KWA UPANGA NAWE UTAULIEA KWA UPANGA, TAFITI HIZI ZINAONYESHA SI RAHISI KUZUIYA MKUKI KWA SHUKA