Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WEMA, IDRIS MAHABA NIUE!

WAANDISHI WETU
WAPENZI? Kwa mara nyingine Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu amesababisha kichwa cha habari kufuatia kunaswa ‘live’ usiku mnene akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan wakioneshana vitendo vya ‘nakupenda tu’ mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
NI ESCAPE ONE MIKOCHENI
Wawili hao walinaswa wakioneshana mahaba niue hayo usiku wa kuamkia Machi 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar walipokuwa wamekwenda kushuhudia shoo kali ya mpambano kati ya Bendi za The African Stars ‘Twanga Pepeta’ na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.PICHA LILIVYOANZA
Awali, paparazi wetu aliyeamua kulivalia njuga tukio hilo alimshuhudia Wema akiingia ukumbini humo akiwa sanjari na kampani yake, akiwemo shosti wake mkubwa kwa sasa, Aunt Ezekiel na mshauri wake  kikazi, Petit Man.
Walikwenda kukaa kwenye viti vilivyokaribiana na kuanza kufuatilia mpambano wa bendi hizo mbili kubwa nchini uliokuwa ukiendelea jukwaani kwa kishindo kikuu.
Idris akimweleza jambo Wema Sepetu.
PETIT AKAA NA MADAM
Kutokana na mpangilio wa watatu hao, Petit Man alikaa katikati ya Wema (kushoto kwake) na Aunt, lakini muda mwingi alikuwa akinong’onezana na Madam huyo huku wakionekana kuzungumza mawili matatu yahusuyo mpambano huo unavyoendelea.
IDRIS NDANI YA NYUMBA
Ndani ya dakika kama ishirini tangu Wema na msafara wake waingie ukumbini humo, Idris naye aliwasili akiwa ameongozana na mdogo wa hiari wa Wema aitwaye Bite pamoja na mtu mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Nao walikwenda walipokuwa wamekaa akina Wema.
ONA HII SASA
Kuonesha kwamba itifaki inazingatiwa, Idris alipofika mahali hapo, Petit alisogeza nyuma kiti chake na kuwafanya Wema na Idris waweze kukaribiana na kuzungumza kwa ujirani zaidi.
Wakipozi kimahaba.
WAANZA KUNONG’ONEZANA
WAFUTANA JASHO
Kama vile hiyo haitoshi, ilifika mahali Wema alionekana usoni kuvuja jasho kwa mbali, basi alichukua skafu ya Idris kutoka shingoni na kujifuta ambapo Idris naye alimsaidia na baadaye Wema naye alifanya vivyo hivyo pale mwenzake huyo naye alipotokwa na jasho.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
“Mh! Mwenzangu we acha tu. Hii ndiyo inaonesha sasa Wema na Idris kuna kitu, maana siku za hivi karibuni, kila alipokuwa anakwenda Wema, Idris naye alikuwa hakosi sasa leo hapa ndiyo full mahaba niue, hatari,” alisikika mpenda ‘ubuyu’ mmoja.
PICHA ZINAJIELEZA?
IDRIS AGOMA KUZUNGUMZA
Jitihada za kuzungumza na Idris ziligonga mwamba kutokana na staa huyo wa BBA aliyejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani laki tatu (zaidi sh mil. 514) kutokuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na ukaribu wake na Wema ukumbini hapo.
 
Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
MUDA WA KUONDOKA WAFIKA, WAONDOKA PAMOJA
Wakati shoo ikielekea ukingoni, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiongozana  katika msafara mmoja na Aunt, Petit na Bite ambapo walitokomea kusikojulikana.

PENNY: USISTA DUU UTATUMALIZA


ALIYEKUWA mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa tabia ya baadhi ya wasichana mastaa kujiona masista duu itawamaliza kwa sababu watajikuta uzee unawakabili bila kuwa na ndoa.
Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, Peniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza na gazeti hili, Penny alisema mastaa wengi wanapenda kujiona ni matawi ya juu na kufikia hatua ya kudharau watu wengine kiasi kwamba hata wenye mapenzi ya dhati kwao hujikuta wakijiweka pembeni hivyo kuwafanya ‘kuchina’ wakati wakitafuta ndoa.
“Unajua kuna vitabia fulani hivi mastaa tunavyo, ya kisista duu ambayo inatufanya tuchine, maana wengi si wanatuogopa wakidhani sisi ni matawi ya juu wakati ni wa kawaida sana,” alisema Penny.

UNYAGO WA KICHINA NA WANAWAKE WA KISASA, BALAA TUPU

Kama kawa nimerudi tena nikiwa na hasira kama faru aliyejeruhiwa, nakuuliza hivi kwa nini lakini? Tabia hiyo ndo uliyofundwa mkoleni? Jamani kabila lako si ndiyo  mafundi wa kuwaweka ndani wanawari, mnafundishwa nini, kuogea machicha ya nazi?
Loh! Mwana mbona unatia aibu kabila lako? Unamuaibisha somo yako na kuonekana mafunzo yote aliyokupa ulipokuwa mkoleni kazi bure.Jamani hivi ewe mwana, kutulia kwako kuna nini? Nyumba yako ina moto kila kukicha kiguu na njia na kusababisha kulichafua kabila lako na kuonekana kama mtu akioa kabila hilo kauoa moto. Sifa nyingine mbaya kuongea kama umemeza kanda, jamani nani aliyekufunda mkoleni kwamba mwanamke anazungumza kuliko mwanaume? Wewe mtoto wa kike umeolewa lakini mtu akikuangalia ulivyo anajua wewe ni changudoa, jamani mbona aibu, natamani kulia na kujiuliza hawa masomo wa sasa ni wakosa haya wasiojua nini maana ya mafunzo ya kumuandaa mwanamke.
Haya hukushika mafunzo ya kuishi na mwanaume hata uanamke wako huujui?
Mungu wangu! Yote tisa kumi ingia kwenye kicheni pati za sasa uozo mtupu, mwanzo zilivyoanza kwa kweli zilikuwa zikizingatia maadili kwa mtu aliye ndani ya ndoa yake kumfunda mwari japo nayo haikutosha kwa vile mafunzo ya kumuandaa binti huchukua zaidi ya mwezi mmoja.
Lakini leo inatisha, mpaka kuna kipindi huwa namuomba Mungu atusamehe kwa vile uchafu tunaofanya kwenye kicheni pati zetu matokeo yake ndoa zimekuwa mnaoana asubuhi mnaachana jioni.Sasa hivi umekuwa unyago wa Kichina kila mtu ana ruksa kuingia na kusema, na anayeelezwa yanaingilia kulia yanatokea kushoto akitoka ana yake basi ndani ya nyumba balaa tupu. Jamani hii kali inafikia hatua eti watu wanamchukua shoga (mwanaume si riziki) kwenda kumfunda mwari, jamani hii ni laana au nini. Mbona tumekuwa tunautia najisi uanamke wetu.
Leo hii wanawake tumeshindwa kufundana wenyewe tunawaita mashoga. Hii si laana na kutufanya kila kukicha wanawake tupoteze maadili na nyumba zetu kuwa kama kaa la moto hazikaliki.
Hivi jamani huyo shoga anajua usafi wa mwanamke akiwa katika siku zake afanye nini? Kuna wanawake wengi leo hii hawajui wakiwa katika siku zao wafanye nini na uchafu wao wauhifadhi vipi. Sasa hivi kicheni pati imekuwa ndiyo sehemu ya watu kukaa utupu na kutukana kila neno baya kusemwa ndani ya kicheni pati.Kingine kinachochekesha ni pale unampa mtu asiyeijua ndoa kumfunda anayetaka kuolewa. Mtaani ana sifa mbaya kishata mtaa, yeye tambara la deki, yeye jamvi la wageni ndiyo unampa kipaza sauti amfunde muolewaji. Jamani eeh!  Usiyoionja huijui ladha yake, mwenye ndoa ndiye atakueleza ndoa ipo vipi.
Mwari ndoa ina mambo mengi ndoa bila uvumilivu hukai, haya huyo kishata mtaa atayajuaje kama siyo kuyasema asiyoyajua. Kuna ndoa leo hii ukiambiwa ina miaka hamsini lakini ndani yake kuna kila aina ya taabu na raha, maumivu na furaha lakini yote walivumiliana na kuwafanya wawe mfano bora wa kuigwa. Hebu mtu huyo asimame au akufunde kwa wakati wake utagundua vitu vingi ambavyo vitakufanya uijue ndoa kiundani. Jamani ukiingia ndani ya ndoa unatakiwa utulie ubadilike uonekane kweli mke wa mtu kwa tabia na mavazi yako. Tulia nyumbani msikilize mumeo toka kwa amri si kila kitu mtaani unakitaka wewe, sherehe gani ipite bila kwenda na kushona sare. Ukinyimwa unadai talaka, shuuutu mwari ndoa mbaya ukiwa nayo ikikutoka utaitafuta mpaka kwa waganga.
Hebu basi tutumie mafunzo ya unyagoni tuzilinde nyumba zetu pia tuufahamu uanamke wetu ili tufute ile dhana mbaya wanawake mwalimu wetu kipofu, kwa mambo yanayoendelea naona mwalimu wetu hana kichwa kabisa. Yangu nimemaliza.

Faraja Kota Nyalandu 'Sio Lazima Ujue Kila Kitu Kila Wakati na Hutokaa Ujue Kila Kitu Kila Wakati'

Sio wakati wote utakuwa na majibu. Sio wakati wote utajua kama unapatia au unakosea. Sio wakati wote utakuwa na uhakika. Ninachotaka kukuambia ni kuwa; it is okay. Si lazima ujue kila kitu kila wakati. Na hautokaa ujue kila kitu kila wakati (translation: don't be self-righteous). But it's okay. Tujue mipaka yetu, tujue uwezo wetu na tujue mapungufu yetu. Tujitambue. Tujikubali. Tuanze kujiboresha kuanzia hapo. But put your worries to rest because it's okay, we are human beings afterall...here is one of my favourite lines: Feel the fear and do it anyway! P. S 

Kutongoza Wanawake Walioolewa ni Rahisi Kuliko Wasioolewa..

Hili sasa halina mjadala au ubishi kuwa kumtongoza mke wa mtu ni rahisi sana kama kusukuma tairi katika mteremko wa mlima kitonga. Lakini ni ngumu mno kutongoza hawa wasichana wetu wa kiswaz wana mlolongo mrefu na usumbufu.

Kwanini hali hii?

Karibuni

ESTER: BABA MZAZI ALINIKATAZA KUIGIZA


LEO hii kwenye Live Chumba cha Habari ya Global Publishers tunaye msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Ester Kiama ambaye pia ni mjasiriamali anayejishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ya kuuza mkaa, pikipiki na magari.
Msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Ester Kiama akisisitiza jambo.
Katika mahojiano na safu hii huku akirekodiwa na timu nzima ya Global TV Online , Ester alisema hapendi watu wamjue mpenzi wake kwani anaogopa kuibiwa na wasichana wa Dar es Salaam kwa hiyo hapendi kumtangaza kabisa.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo pia yanapatikana katika Kipindi cha Exclusive Interview kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com kitakachorushwa leo.
Mwandishi: Nini kilikusukuma mpaka ukawa muigizaji?
Ester: Nilikuwa napenda sanaa tangu nikiwa mdogo na zamani nilishajaribu kutaka kuigiza enzi hizo za Kibakuli na Muhogo Mchungu, nikawa naenda kuangalia wanavyofanya mazoezi pale Magomeni (jijini Dar) lakini baba yangu hakupenda na walijaribu kuja kuniombea nianze na mimi kuigiza baba yangu akawatimua akasema hataki kusikia hata kidogo kwa hiyo nikashindwa kwa sababu wazazi wangu walikuwa wanataka nimalize shule kwanza.
Mwandishi:  Umecheza filamu ngapi mpaka sasa hivi na una filamu ngapi za kwako mwenyewe?
Ester: Nimecheza nyingi kama kumi na moja na filamu ambayo imenitambulisha ni ile ya Profesa ambayo iko mtaani sasa hivi, filamu ambayo nimecheza vizuri ambayo huwa sichoki kuiangalia ni filamu yangu mwenyewe inayoitwa Ngoma Ngumu.
Ester Kiama akipozi.
Mwandishi: Ulimfahamu vipi Dude?
Ester: Dude nilikutana naye kwenye filamu yangu ambayo nimeiongoza ya Ngoma Ngumu, nilimuita aje acheze kwa sababu nilivyosoma ile stori ya filamu nilihisi ile sehemu inamfaa, akaja nyumbani nikamuona na ndiyo tukaanzia hapo lakini mwisho wa siku nikaona anafaa kuwa rafiki kwa sababu aliniongoza katika hiyo filamu.
Mwandishi: Ukaribu wako na Dude ukoje?
Mwandishi: Unakabiliana vipi na maneno yanayosemwa kuwa wewe na Dude ni wapenzi?
Ester: Ni jambo gumu kidogo, na siyo kwangu au kwa mpenzi wangu lakini kwa upande wa Dude pia kwa sababu naye si ana mke kwa hiyo pia ni jambo gumu na watu kuelewa ni ngumu zaidi lakini mwisho wa siku mpenzi wangu ananielewa.
Mwandishi: Umeolewa au una mpenzi?
Ester: Sijaolewa lakini nina mpenzi, siwezi kumtaja kwa jina kwa sababu sipendi watu wamjue na ninaogopa kuibiwa na wasichana wa Dar es Salaam wanaiba sana wanaume za watu.

Demi Lovato Shows Off Puppy, Bikini Body

 Demi Lovato Bikini Photo
Demi Lovato has unveiled a new Instagram photo that is both totally adorable AND drop dead sexy.
It features the 22-year old singer holding her puppy while flaunting her impressive bikini body, writing as a caption to the image... nothing. She just included a sun, palm tree and heart emoji.
Lovato, of course, spent many weeks in rehab a few years ago, partly over substance abuse issues and partly due to a battle with bulimia.
There was simply no way the old Demi Lovato would have posted a photo such as this.
But now?
"I love my butt," Lovato recently told Allure. "Hopefully it stays that way, because this thing isn't going anywhere."
About a month ago, meanwhile, Demi posted another swimsuit snapshot, writing along with it an empowering message to young women everywhere.
“Regardless of what society tells you these days… You don’t have to have a thigh gap to be beautiful," she penned, adding:
"It is possible to love your body the way it is. #fitness #health #acceptance #selflove."
Amen, sister.
Lovato also considers herself lucky for waking up alongside Wilmer Valderrama every morning.
Along with a cute photo of the couple, Lovato wrote on Instagram a few weeks ago:
"After sharing my ups, putting up with my downs and supporting my recovery... he still never takes credit and I want the world to know how incredible his soul is. I really wouldn't be alive today without him. I love you Wilmer."

SHOGA: CHAKULA CHA USIKU KISILIWE GIZANI!

 
Asalaam alaykhum shoga yangu! Kama ilivyoada, leo ni Jumanne nyingine ambayo Mwenyezi Mungu amependa tukutane tukiwa wenye afya njema.Binafsi namshukuru kwa mapenzi yake kwangu kwani wapo wenzetu wanasumbuliwa na maradhi na matatizo lukuki ikiwemo misiba.
Shoga yangu, baada ya wiki iliyopita kuelezea namna ya kucheza na maeneo flani ya waume zetu ili kuwapa mushawasha wa mahaba nao kutuburudisha, leo nitazungumza nawe kuhusu madhara ya kumpa mumeo chakula cha usiku gizani.
Nimeamua kuliongelea suala hili kwa sababu wapo wenzetu wanapokula chakula cha usiku huzima taa, wanashangaza kwa kweli!Shoga yangu, kabla sijasonga mbele hebu nikuulize, hivi unapompa mumeo chakula cha usiku kwenye giza unamuogopa, unaona aibu au inakuwaje?
Sasa shoga yangu mwenye tabia hiyo ngoja leo nikuambie ukweli kwamba ukitaka kufurahia chakula cha usiku kiliwe kwenye mwanga wa kutosha.Raha ni pale utakapokuwa na mumeo mnakula chakula hicho kila mmoja wenu avione viungo vyote vya mwenzake.
Kitendo cha mumeo kuiona midomo, macho yako na maeneo mengi ya mwili wako kitamfanya afurahie chakula chako na kupata hamasa ya kupenda kula nawe kila siku.
“Siyo siri mke wangu, kama siku zote ungekuwa unanipa chakula cha usiku kwenye mwanga wa kutosha kama leo, ningenenepaje?” mumeo hata kama hana tabia ya kukusifia atafunguka tu.
Halikadhalika, hata wewe kitendo cha kuona midomo ya mumeo inavyocheza na macho yake yakiwa hayabanduki usoni kwako na kama mumeo mtundu, wakati huo wa chakula cha usiku atakukonyeza, hakika utajisikia raha ya kupitiliza.
Mtu asikudanganye shoga yangu, hakuna kitu kitamu kama kula chakula cha usiku kwenye mwanga wa kutosha kwani kila mmoja atajiachia atakavyo kwa mwenzake.
Shoga, unapozima taa wakati wa chakula cha usiku unahatarisha ndoa yako, na kwa nini ufanye hivyo wakati uliyemuandalia chakula hicho ni mumeo uliyeahidi kujitoa kwake kwa kila kitu? Kama wewe ni miongoni mwa wanaofanya hivyo hebu leo usiku kula na mumeo chakula cha usiku kwenye mwanga wa kutosha.
Wakati mnakishambulia chakula hicho usiwe na papara, naamini atakushika hata kwenye maeneo ambayo alikuwa hayagusi kabisa nawe utafurahia kuwa naye na kujiona ulikuwa unakosa vitu adimu maishani mwako. Bye!
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

AMANDA AZIDIWA, ASHINDWA KUMZIKA MEZ B


MREMBO kunako tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ ameshindwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moses Bushagama aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Dodoma kutokana na kuugua ghafla.
Mrembo kunako tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’.
Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko, Amanda ambaye pia ni mtu wa karibu na marehemu, alisema kuwa alishapanga kusafiri kwenda Dodoma kwa ajili ya maziko lakini kitendo cha kuugua ghafla kimeharibu kila kitu.
“Imeniuma sana kwa sababu ya ugonjwa wa taifodi kuniandama ambapo nilikuwa nikitapika mfululizo,” alisema Amanda.Mez B alikuwa akiumwa ugonjwa wa homa ya mapafu, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mwananchi kabla ya umauti kumkuta. Amezikwa Jumatatu katika makaburi ya Wahanga mkoani Dodoma.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

JOYCE KIRIA ADAIWA MILLION 500


MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia  kipindi chake.
 
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
Akiongea na Uwazi, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.
Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Picha za Show Nzima ya Yamoto Band Iliyofanyika Huko London Katika Ukumbi wa Royal Regency

Vijana wa Yamoto Band jumamosi iliyopita Walipiga Bonge moja la Show huko UK London katika Ukumbi wa Royal Regency na kuhudhuliwa na watu kibao wanaoishi huko, Hizi ni picha za matukio katika Show Hiyo.








Mbuta Nanga nae Alikuwepo.....
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

MANAIKI: SIJAKATA TAMAA KUMUOA WALPER


MSANII filamu za Kibongo, Manaiki Sanga amefungukai kuwa hajakata tamaa kumuoa msanii mwenzake, Jacqueline Walper na kwamba bado anaendelea kuwashawishi wazazi wake.
 
Msanii filamu za Kibongo, Manaiki Sanga akiwa na msanii mwenzake, Jacqueline Walper.
Akichezesha taya na Uwazi, Manaiki aliweka wazi kuwa bado anawashawishi wazazi wake wakubaliane na uchaguzi wake kwakuwa ndiye mtu anayempenda.
“Ni upande mmoja tu wa ndugu zangu ambao wapo kijijini Mbeya na hawamfahamu Walper ila sijakata tamaa na naamini watanielewa tu kwa maaana ndoto yangu mimi ni kumuoa mtu ambaye ninampenda,” alisema Manaiki.
Hivi karibuni Manaiki alitangaza nia ya kumuoa Walper ambapo wazazi wake walimkatalia na kumwambia atafute msichana wa kutoka mkoa wake.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

IYOBO ASHIKWA NA KIGUGUMIZI KUHUSU MUME WA AUNT


DANSA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ameshikwa na kigugumizi kuhusu tuhuma za kumpachika mimba Aunt ambaye ni mke wa mtu.
 
Dansa wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo akiwa na Aunt Ezekiel.
Mose alionesha kigugumizi hicho baada ya kutaitiwa na paparazi wetu akiulizwa anajisikiaje kumpachika mimba mke wa mtu na vipi kama mume wa Aunt anayedaiwa kufungwa huko Dubai ataachiwa huru na kurudi.“Aaahhaa.. Mhh..Hayoo ni ya Aunt mwenyewe mimi hayanihusu,” alisema Mose kisha kimya kirefu kikafuatia kabla ya kuikata simu yake.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Faiza: Kuwa Mama Poa Sana, Natamani Nizae Team ya Mpira!!

Mwigizaji wa filamu mwenye vituko vya aina yake, Faiza Ally ambae ni mama wa mtoto moja, aliezaa na Mbunge wasasa wa Mbeya mjini, ameyasema hayo  akiwa visiwani Zanzibar kwenye mapumziko mafupi.

Mwigizaji huyu ambae mara kabdhaa amekuwa akijisifia kwa kuwa na FIGA nzuri akidai hata baada ya kuzaa bado umbo na mvuto wake bado upo pale pale amesema angekuwa na uwezo wa kipesa  angezaa watoto wengi zaidi kiasi cha kufikisha idadi ya wachezaji wa timu ya mpira kwa sababu kuwa mama ni kitu kizuri sana kwake.

Kuwa mama ni kazi poa sana- naipenda sana yaani ningekua na uwezo wa kipesa ningezaa team ya mpira
Mbali na watu kuendelea kumshambulia kuhusu uvaaji wa nguo zake akiwa na mtoto wake mwananamama huyu ameonekana ni mtu mwenye kufanya kile anachokiamni  na sio watu wanataka nini.
Jionee baadhi ya picha hapo juu akiwa na mtoto wake ufukweni.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

PENINA KUPIGWA NDOA MUDA WOWOTE


MUIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Jennifer Raymond ‘Penina’, amefunguka kuwa anatarajia kufunga ndoa muda wowote kuanzia sasa.
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Jennifer Raymond ‘Penina’.
Akizungumza na Uwazi, Penina alisema kuwa harakati za kuolewa zipo jikoni hivyo anamuomba Mungu kile ambacho kinatarajia kufanyika kiweze kwenda kama alivyopanga ingawa hakutaka kumweka wazi mwanaume huyo kwa madai kuwa hataki kuibiwa.
“Mambo ya ndoa yapo tayari na anayesubiriwa ni mwanaume ambaye anataka kunioa ili alete barua ya uchumba, kwa sasa yuko nje kwa ajili ya mambo yake binafsi lakini atakapotua tu Bongo, muda wowote ndoa itafungwa,” alisema.
 USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Akina Dada huu utaalamu utawacost sana: hivi inakuwajue unaweka viungo sehemu za siri kama pilau?

Nimekutana na huyu dada anaomba ushauri kwa Joyce Kiria
Miaka 3 ilopita nimekuwa katika matatizo makubwa sana.....nawashwa sana sehemu za siri (uken). nilienda baadhi ya hospitali wanasema ni fungus nikatumia dawa baada ya wiki tatizo likajirudia. Nimekuwa mtu wa kujikuna wakati wote. Ukeni panawaka moto kwa kujikuna, nimeendelea na tiba mpaka likaibuka tatizo jingine . kila ninapofanya tendo la ndoa napata maumivu ambayo hayaelezeki wakati mwingine mpaka naanza kubleed.
Kurudi tena hospitali wakasema nipime vipimo vya kansa lakini tatizo likazidi kuongezeka na sasa siwezi hata kufanya tendo la ndoa. madaktari ktk vipimo wakagundua kwenye uk-e kuna wekundu mwingi sana badala ya rangi ya pink. 
Kumbe ile rangi nyekundu ni sehemu ambayo imeshambuliwa na bacteria wasiosikia dawa. Wakajaribu kupeleka dawa sehemu iliyoathirika bado ikashindikana kuwaua!
Baadae madaktari wa Muhimbili wakaniuliza ninavyofanya usafi katika sehemu zangu za siri na nikawambia ukweli kwamba, "NASAFISHA KWA KUINGIZA VIDOLE NDANI, NAJIINGIZA ASALI NA PAMBA NDANIILI UKKE UWE UMEBANA NA VINGINE VINGI tu tunavyoshauriana na wasichana (VIUNGA SEHEMU ZA SIRI).
Madaktari wakasema sababuya tatizo langu nimeua bakteria wote walinzi ndani ya ukke ndo maana nimmeshambuliwa na bacteria ambao hawaskii dawa
Ndugu zangu nilikuwa nikiunga sehemu za siri (ukke) kwa VIUNGO na naingiza kucha pamoja na sabuni ili uwe ubane na upendeze. Sasa nimeshauriwa nitoe kizazi katika umri wa miaka 29 kwani nikiacha itakuwa kansa. Najua mna ndugu zenu wa kike au wake zenu. Wape tahadhari juu ya hili.
My take: Hivi hadi uweke asali, vidole, pamba nk ndani ya ukkke ili ubane unatafuta nini? Kuna mashindano ya zinazobana, na wanawapa tuzo gani hadi utake risk kias hiki?
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Le Projectii:Wema Sasa Ampikia na Kumpakulia Ommy Dimpoz

Wakati mwanamziki wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz akiendelea kupepesa macho na kutikisa masikio kukanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwingizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ukaribu wao bado unatia mashaka na kuendeleza sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wapambe wao.

Japo kuwa Ommy alielezakuwa yeye na Wema ni marafiki toka kitambo kabla hata ya wema kuwa na mahusiano na mwanamziki Diamond, lakini  hii imezidiii.

Mbali na kuonekana wawili hawa kuwa pamoja sehemu mablimbali za starehe toka Ommy atoke Marekani, hili la kupikiwa na kupakuliwa nyumbani kwa Wema ndio limezidi kuchochea hisia kuwa wawili hao wanamahusiano zaidi ya USHKAJI.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwanadada Wema ambae na folloers zaidi ya laki nne , alibandika picha hiyo hapo juu akionekana kumpakulia chakula ambacho alijisifia ni kizuri na amekipika mwenyewe na kumtania Ommy kuwa alikuwa analeta pozi kwenye kula.

“Dat moment anapokuja home and umepika chakula alafu analeta pozi at first then unashangaa anaenda sahani mbili.... Talk About Good Food Made Real Good”- Wema aliandika mara baada ya kutupia picha hiyo.

Japo kuwa hadi sasa mwanadada Wema Sepetu ajajitokeza kukataa au kukubali juu ya yeye kuwa na mahusiano na Ommy lakini idadi kubwa ya wampambe wake mitandaoni na ifagilia sana hii “Couple”.

Tuvute subraaa.

Mzee wa Ubuyu
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Mrembo wa Nguvu Jokate Atupia picha zake Mpya za Kumtoa Nyoka Pangoni

 Mrembo Jokate Ameshare nasi Picha zake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram ..
Toa Maksi zako out of 10

 
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Jibu la Amber Baada ya Kanye West kusema alibidi aoge mara 30 ili kuwa na Kim Kardashian baada ya kuwa na Amber Rose.

Kwenye mahojiano na kipindi cha ‘BreakFast Club’ Kanye West alimkejeli mpenzi wake wa zamani Amber Rose kwa kusema alibidi aoge mara 30 baada ya kuwa naye ili Kim kardashian awe naye.

Kanye West alisema “Kim k angekubali kuwa na mimi kabla ya Amber basi nisinge kuwa na Amber Kabisa, ni ngumu kwa mwanamke kuwa na mwanaume aliyewahi kuwa na mahusiano na Amber, nilibidi nioge mara 30 ili Kim K anikubali”.

Amber amejibu kupitia twitter yake nakusema …



USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

PICHA: Uwoya aonyesha Tatoo yake ili watu waisome?

Vijimambo: Picha hii ya mrembo na mwigizaji  wa filamu anaezimikiwa na mashabiki wengi, Irene Uwoya imewaacha midomo wazi mashabiki wake huku wakiwa na alamaza kujiuliza vichwani mwao.

Irene aliibandika picha hii  mtandaoni bila kuandika kitu chochote kwahiyo ikawa kawa amewaachia fursa mashabiki wake watiririke.

Mbali na watu kusifia uzuri wake kwa ujumla, watu wengi walijikita kwenye tattoo yake ambayo amejichora juu ya kifua, karivu kabisa na shingo yake.

Wengi walijiongeza kuwa mwanadada huyu ameionyesha tattoo hiyo ili watu waweze kusoma ni nini alichokiandika, na wapo walio jaribu kuandika kile kilichoandikwa hapo.

Kiukweli mimi macho yangu hayako vizuri, mwenye macho tunaomba umtusidie, ameandika nini hapo?.

Mzee wa Ubuyu
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top