Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

ESTER: BABA MZAZI ALINIKATAZA KUIGIZA


LEO hii kwenye Live Chumba cha Habari ya Global Publishers tunaye msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Ester Kiama ambaye pia ni mjasiriamali anayejishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ya kuuza mkaa, pikipiki na magari.
Msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Ester Kiama akisisitiza jambo.
Katika mahojiano na safu hii huku akirekodiwa na timu nzima ya Global TV Online , Ester alisema hapendi watu wamjue mpenzi wake kwani anaogopa kuibiwa na wasichana wa Dar es Salaam kwa hiyo hapendi kumtangaza kabisa.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo pia yanapatikana katika Kipindi cha Exclusive Interview kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com kitakachorushwa leo.
Mwandishi: Nini kilikusukuma mpaka ukawa muigizaji?
Ester: Nilikuwa napenda sanaa tangu nikiwa mdogo na zamani nilishajaribu kutaka kuigiza enzi hizo za Kibakuli na Muhogo Mchungu, nikawa naenda kuangalia wanavyofanya mazoezi pale Magomeni (jijini Dar) lakini baba yangu hakupenda na walijaribu kuja kuniombea nianze na mimi kuigiza baba yangu akawatimua akasema hataki kusikia hata kidogo kwa hiyo nikashindwa kwa sababu wazazi wangu walikuwa wanataka nimalize shule kwanza.
Mwandishi:  Umecheza filamu ngapi mpaka sasa hivi na una filamu ngapi za kwako mwenyewe?
Ester: Nimecheza nyingi kama kumi na moja na filamu ambayo imenitambulisha ni ile ya Profesa ambayo iko mtaani sasa hivi, filamu ambayo nimecheza vizuri ambayo huwa sichoki kuiangalia ni filamu yangu mwenyewe inayoitwa Ngoma Ngumu.
Ester Kiama akipozi.
Mwandishi: Ulimfahamu vipi Dude?
Ester: Dude nilikutana naye kwenye filamu yangu ambayo nimeiongoza ya Ngoma Ngumu, nilimuita aje acheze kwa sababu nilivyosoma ile stori ya filamu nilihisi ile sehemu inamfaa, akaja nyumbani nikamuona na ndiyo tukaanzia hapo lakini mwisho wa siku nikaona anafaa kuwa rafiki kwa sababu aliniongoza katika hiyo filamu.
Mwandishi: Ukaribu wako na Dude ukoje?
Mwandishi: Unakabiliana vipi na maneno yanayosemwa kuwa wewe na Dude ni wapenzi?
Ester: Ni jambo gumu kidogo, na siyo kwangu au kwa mpenzi wangu lakini kwa upande wa Dude pia kwa sababu naye si ana mke kwa hiyo pia ni jambo gumu na watu kuelewa ni ngumu zaidi lakini mwisho wa siku mpenzi wangu ananielewa.
Mwandishi: Umeolewa au una mpenzi?
Ester: Sijaolewa lakini nina mpenzi, siwezi kumtaja kwa jina kwa sababu sipendi watu wamjue na ninaogopa kuibiwa na wasichana wa Dar es Salaam wanaiba sana wanaume za watu.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top