

Miss Jamaica Kaci Fennell (22) aliyetarajiwa na wengi kutwaa taji hilo.




Mashabiki
wa Miss Jamaica baada ya matokeo hayo walivamia mitandao ya kijamii
ikiwemo Twitter kumtangaza mrembo huyo aliyejipatia umaarufu pengine
zaidi ya mshindi.
MISS Colombia, Paulina Vega atwaa taji la Miss Universe 2015 katika
fainali zilizofanyika jana huko Miami nchini Marekani huku umati
ukizomea kuonyesha kutoridhika na matokeo hayo.Umati uliohudhuria fainali hizo ulitarajia Miss Jamaica Kaci Fennell aliyeshika nafasi ya nne kutwaa taji hilo lakini ulionyesha kushangazwa na maamuzi ya majaji kumtangaza Miss Colombia Paulina Vega mwenye miaka 22.
Zomea zomea zilisikika mara baada ya mshindi huyo kutangazwa huku kukiwa na minong'ono ya hujuma katika mashindani ya mwaka huu.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI