

Zamani ilikuwa kawaida kukuta kijiwe cha kahawa kinaanza asubuhi hadi usiku, siku hizi ni vijiwe vya kuhesabu na hata wanaokaa kutwa nzima kijiweni wanazidi kupungua, ingawa idadi kubwa ni watu wenye umri mkubwa. Vijana wanapungua vijiweni kwa sababu wameshagundua hakuna mtu wa kuwasaidia maisha yao pasipo wenyewe kwenda spidi.

Shiriki umbeya, kwa sababu wakati mwingine hauwezi kuukwepa, lakini kuwa na akili ya ziada. Siyo kila utakaloambiwa ni baya, hapana.
Yapo mengine ni mazuri, yaweke na yafanyie kazi, lakini nina uhakika, kwa asilimia zaidi ya 80, wanawake wanaongea mambo yasiyowasaidia, yaani huyu ana vile, yule ana hivi, wale wanafanya hivi na mambo mengine kama hayo.
Usiwasikilize na kuwaamini. Jione kama uko peke yako na kila anayekuzunguka ni adui. Kuwa makini na unachokiongea mbele yao, na usiwe wakala wa kusambaza kinachozungumzwa nao. Ukiwa hivi, utajiweka salama.
Na hata ukiletewa umbeya, kwamba unasemwa vibaya na huyu, usiwe na haraka ya kuamua mambo, wakati mwingine kusemwa vibaya na kuyaacha kama yalivyo ni baraka.Ila nikusisitize kitu kimoja, mwanamke ana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kimaisha duniani kuliko mwanaume, kwa sababu amepewa kila kitu, hasa uwezo wake wa kumshawishi mwanaume amsaidie kufikia ndoto zake!
Karibuni
sana wasomaji wangu wapendwa katika safu hii maalum kwa ajili ya
kuelekezana mambo mbalimbali yanayohusu maisha kwa ujumla hasa upande wa
mapenzi kama siyo mahaba.Mfano wa mambo hayo ni namna wenza wanaoishi
na ndugu au wazazi wao wanavyopaswa kuishi kwa hekima bila kuwakwaza.
Kujiepusha
na kauli zisizofaa ambazo mara nyingi zimekuwa zikiharibu uhusiano wao,
kujiweka katika mazingira ya usafi wa nyumba na mavazi.Mambo mengine ni
kuwa waaminifu katika uhusiano wao kwa sababu wenza wakiwa na michepuko
huweza kuleta maradhi ndani ikiwa ni pamoja na migogoro inayosababisha
kuachana.







