
Mshambuliaji Emmanuel Okwi akibebwa baada ya kuzimia.
MOYO wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ulisimama kwa sekunde kadhaa alipogongwa kisogoni na beki Aggrey Morris wa Azam FC.
Okwi aligongwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC
iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, jana.Daktari wa Simba, Yassin Gembe, amesema moyo wa Okwi
ulisimama kwa sekunde kadhaa kutokana na pigo la kisogoni karibu kabisa
na ubongo katika eneo la Medullar Oblangata.
“Hakikuwa kitu kidogo, tulilazimika kufanya tiba ili kurudisha mapigo
ya moyo wake kwa kuwa ulisimama kwa sekunde kadhaa. Aliumia na uliona
akitoa mapovu. “Baada ya hapo, tuliona ni vema kumfikisha Muhimbili
ambako vipimo vyote vimefanyika. Imeonekana hakuumia sana na
ameruhusiwa.
“Lakini mimi nimeamua kumpumzisha kwa siku mbili ili kuangalia kama
atakuwa katika hali gani maana mwanzo unaweza kuona yuko vizuri kumbe
kuna tatizo. “Ikionekana anaendelea vizuri, basi ataanza mazoezi lakini
atakuwa chini ya uangalizi wangu,” alisema Dk Gembe.
Mshambuliaji wa Simba, Dan Sserunkuma alitumia muda mwingi kumlaumu
Morris kwamba alishiriki kumpiga Okwi kiwiko, hata hivyo, alikuwa
akikanusha.Okwi alibebwa haraka na kutolewa uwanjani na baadaye
kukimbizwa Muhimbili ikiwa ni baada ya kuzinduka.
Kugongwa huko kwa Okwi, jana jioni kulizua gumzo kwa mashabiki wa
soka nchi hasa wa Simba ambao walikuwa wakipiga simu katika ofisi za
gazeti hili wakidai mabeki wamekuwa wakatili kwa washambuliaji.
Wengi walitolea mfano wa beki George Michael wa Ruvu Shooting kumkaba mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI