Labda ni mimi tu ila kinachoendelea Azam Tv Kwenye Hizi fainali za AFCON
kinaboa sana , yaani ile Chanel ya Azam 2 ambayo tulitegemea ituletee
uhondo huo wa mpira haifanyi hivyo badala yake imeweka wachambuzi ambao
wanaongea tu dakika tisini bila kuonyesha mpira wenyewe unaochezwa,
kibaya zaidi kuna Kituo kimoja katika package ya Azam tv inayoitwa UBC
siku mbili hizi Tatu zilikuwa zinaonyesha fainali hizo , leo ukiweka
hiyo channel ya UBC inasema Channel Restricted ikiwa na maana wameizuia
ili tusione mpira kwa maana tuendelee kuwaangalia tu wachambuzi wao wa
Azam 2 bila kuona mpira....
Hivi kituo kikubwa cha michezo kama nyie kweli mmekosa leseni ya kuonyesha huo mpira??
Haingii akilini
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment