Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WEMA, IDRIS MAHABA NIUE!

WAANDISHI WETU
WAPENZI? Kwa mara nyingine Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu amesababisha kichwa cha habari kufuatia kunaswa ‘live’ usiku mnene akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan wakioneshana vitendo vya ‘nakupenda tu’ mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
NI ESCAPE ONE MIKOCHENI
Wawili hao walinaswa wakioneshana mahaba niue hayo usiku wa kuamkia Machi 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar walipokuwa wamekwenda kushuhudia shoo kali ya mpambano kati ya Bendi za The African Stars ‘Twanga Pepeta’ na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.PICHA LILIVYOANZA
Awali, paparazi wetu aliyeamua kulivalia njuga tukio hilo alimshuhudia Wema akiingia ukumbini humo akiwa sanjari na kampani yake, akiwemo shosti wake mkubwa kwa sasa, Aunt Ezekiel na mshauri wake  kikazi, Petit Man.
Walikwenda kukaa kwenye viti vilivyokaribiana na kuanza kufuatilia mpambano wa bendi hizo mbili kubwa nchini uliokuwa ukiendelea jukwaani kwa kishindo kikuu.
Idris akimweleza jambo Wema Sepetu.
PETIT AKAA NA MADAM
Kutokana na mpangilio wa watatu hao, Petit Man alikaa katikati ya Wema (kushoto kwake) na Aunt, lakini muda mwingi alikuwa akinong’onezana na Madam huyo huku wakionekana kuzungumza mawili matatu yahusuyo mpambano huo unavyoendelea.
IDRIS NDANI YA NYUMBA
Ndani ya dakika kama ishirini tangu Wema na msafara wake waingie ukumbini humo, Idris naye aliwasili akiwa ameongozana na mdogo wa hiari wa Wema aitwaye Bite pamoja na mtu mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Nao walikwenda walipokuwa wamekaa akina Wema.
ONA HII SASA
Kuonesha kwamba itifaki inazingatiwa, Idris alipofika mahali hapo, Petit alisogeza nyuma kiti chake na kuwafanya Wema na Idris waweze kukaribiana na kuzungumza kwa ujirani zaidi.
Wakipozi kimahaba.
WAANZA KUNONG’ONEZANA
WAFUTANA JASHO
Kama vile hiyo haitoshi, ilifika mahali Wema alionekana usoni kuvuja jasho kwa mbali, basi alichukua skafu ya Idris kutoka shingoni na kujifuta ambapo Idris naye alimsaidia na baadaye Wema naye alifanya vivyo hivyo pale mwenzake huyo naye alipotokwa na jasho.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
“Mh! Mwenzangu we acha tu. Hii ndiyo inaonesha sasa Wema na Idris kuna kitu, maana siku za hivi karibuni, kila alipokuwa anakwenda Wema, Idris naye alikuwa hakosi sasa leo hapa ndiyo full mahaba niue, hatari,” alisikika mpenda ‘ubuyu’ mmoja.
PICHA ZINAJIELEZA?
IDRIS AGOMA KUZUNGUMZA
Jitihada za kuzungumza na Idris ziligonga mwamba kutokana na staa huyo wa BBA aliyejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani laki tatu (zaidi sh mil. 514) kutokuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na ukaribu wake na Wema ukumbini hapo.
 
Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
MUDA WA KUONDOKA WAFIKA, WAONDOKA PAMOJA
Wakati shoo ikielekea ukingoni, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiongozana  katika msafara mmoja na Aunt, Petit na Bite ambapo walitokomea kusikojulikana.

PENNY: USISTA DUU UTATUMALIZA


ALIYEKUWA mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa tabia ya baadhi ya wasichana mastaa kujiona masista duu itawamaliza kwa sababu watajikuta uzee unawakabili bila kuwa na ndoa.
Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, Peniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza na gazeti hili, Penny alisema mastaa wengi wanapenda kujiona ni matawi ya juu na kufikia hatua ya kudharau watu wengine kiasi kwamba hata wenye mapenzi ya dhati kwao hujikuta wakijiweka pembeni hivyo kuwafanya ‘kuchina’ wakati wakitafuta ndoa.
“Unajua kuna vitabia fulani hivi mastaa tunavyo, ya kisista duu ambayo inatufanya tuchine, maana wengi si wanatuogopa wakidhani sisi ni matawi ya juu wakati ni wa kawaida sana,” alisema Penny.

ESTER: BABA MZAZI ALINIKATAZA KUIGIZA


LEO hii kwenye Live Chumba cha Habari ya Global Publishers tunaye msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Ester Kiama ambaye pia ni mjasiriamali anayejishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ya kuuza mkaa, pikipiki na magari.
Msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Ester Kiama akisisitiza jambo.
Katika mahojiano na safu hii huku akirekodiwa na timu nzima ya Global TV Online , Ester alisema hapendi watu wamjue mpenzi wake kwani anaogopa kuibiwa na wasichana wa Dar es Salaam kwa hiyo hapendi kumtangaza kabisa.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo pia yanapatikana katika Kipindi cha Exclusive Interview kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com kitakachorushwa leo.
Mwandishi: Nini kilikusukuma mpaka ukawa muigizaji?
Ester: Nilikuwa napenda sanaa tangu nikiwa mdogo na zamani nilishajaribu kutaka kuigiza enzi hizo za Kibakuli na Muhogo Mchungu, nikawa naenda kuangalia wanavyofanya mazoezi pale Magomeni (jijini Dar) lakini baba yangu hakupenda na walijaribu kuja kuniombea nianze na mimi kuigiza baba yangu akawatimua akasema hataki kusikia hata kidogo kwa hiyo nikashindwa kwa sababu wazazi wangu walikuwa wanataka nimalize shule kwanza.
Mwandishi:  Umecheza filamu ngapi mpaka sasa hivi na una filamu ngapi za kwako mwenyewe?
Ester: Nimecheza nyingi kama kumi na moja na filamu ambayo imenitambulisha ni ile ya Profesa ambayo iko mtaani sasa hivi, filamu ambayo nimecheza vizuri ambayo huwa sichoki kuiangalia ni filamu yangu mwenyewe inayoitwa Ngoma Ngumu.
Ester Kiama akipozi.
Mwandishi: Ulimfahamu vipi Dude?
Ester: Dude nilikutana naye kwenye filamu yangu ambayo nimeiongoza ya Ngoma Ngumu, nilimuita aje acheze kwa sababu nilivyosoma ile stori ya filamu nilihisi ile sehemu inamfaa, akaja nyumbani nikamuona na ndiyo tukaanzia hapo lakini mwisho wa siku nikaona anafaa kuwa rafiki kwa sababu aliniongoza katika hiyo filamu.
Mwandishi: Ukaribu wako na Dude ukoje?
Mwandishi: Unakabiliana vipi na maneno yanayosemwa kuwa wewe na Dude ni wapenzi?
Ester: Ni jambo gumu kidogo, na siyo kwangu au kwa mpenzi wangu lakini kwa upande wa Dude pia kwa sababu naye si ana mke kwa hiyo pia ni jambo gumu na watu kuelewa ni ngumu zaidi lakini mwisho wa siku mpenzi wangu ananielewa.
Mwandishi: Umeolewa au una mpenzi?
Ester: Sijaolewa lakini nina mpenzi, siwezi kumtaja kwa jina kwa sababu sipendi watu wamjue na ninaogopa kuibiwa na wasichana wa Dar es Salaam wanaiba sana wanaume za watu.

TIWA SAVAGE, FLAVOUR, DAVIDO WASHINDWA KUPIGA KURA NIGERIA

Tiwa Savage.
WAKATI wananchi wa Nigeria wakiwa katika zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika juzi na jana, baadhi ya mastaa walishindwa kuhudhuria tukio hilo muhimu kutokana na majukumu mbalimbali.
 
Davido Adeleke.
Miongoni mwa mastaa hao ni mwanamuziki Davido Adeleke, aliyekuwa na shoo kwenye tamasha moja nchini Kenya hivyo hakuweza kupiga kura.
Flavour N'abania.
Mwanamuziki mwingine Flavour N'abania yeye alikuwa jijini London kwenye Tamasha la Dance Afrique. Huku mastaa wengine wakiwemo Tiwa Savage na P Square wakihudhuria tamasha hilo.
 
Toke Makinwa.
Mtangazaji Toke Makinwa yeye alikuwa nchini China wakati wa tukio hilo.
Mwanamuziki Wizkid ni staa mwingine ambaye hakupiga kura kutokana na shoo yake aliyokuwa nayo huko Dubai.
Wizkid.
Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa leo jioni ambapo Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC wanachuana vikali.

AMANDA AZIDIWA, ASHINDWA KUMZIKA MEZ B


MREMBO kunako tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ ameshindwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moses Bushagama aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Dodoma kutokana na kuugua ghafla.
Mrembo kunako tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’.
Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko, Amanda ambaye pia ni mtu wa karibu na marehemu, alisema kuwa alishapanga kusafiri kwenda Dodoma kwa ajili ya maziko lakini kitendo cha kuugua ghafla kimeharibu kila kitu.
“Imeniuma sana kwa sababu ya ugonjwa wa taifodi kuniandama ambapo nilikuwa nikitapika mfululizo,” alisema Amanda.Mez B alikuwa akiumwa ugonjwa wa homa ya mapafu, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mwananchi kabla ya umauti kumkuta. Amezikwa Jumatatu katika makaburi ya Wahanga mkoani Dodoma.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Picha za Show Nzima ya Yamoto Band Iliyofanyika Huko London Katika Ukumbi wa Royal Regency

Vijana wa Yamoto Band jumamosi iliyopita Walipiga Bonge moja la Show huko UK London katika Ukumbi wa Royal Regency na kuhudhuliwa na watu kibao wanaoishi huko, Hizi ni picha za matukio katika Show Hiyo.








Mbuta Nanga nae Alikuwepo.....
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

MANAIKI: SIJAKATA TAMAA KUMUOA WALPER


MSANII filamu za Kibongo, Manaiki Sanga amefungukai kuwa hajakata tamaa kumuoa msanii mwenzake, Jacqueline Walper na kwamba bado anaendelea kuwashawishi wazazi wake.
 
Msanii filamu za Kibongo, Manaiki Sanga akiwa na msanii mwenzake, Jacqueline Walper.
Akichezesha taya na Uwazi, Manaiki aliweka wazi kuwa bado anawashawishi wazazi wake wakubaliane na uchaguzi wake kwakuwa ndiye mtu anayempenda.
“Ni upande mmoja tu wa ndugu zangu ambao wapo kijijini Mbeya na hawamfahamu Walper ila sijakata tamaa na naamini watanielewa tu kwa maaana ndoto yangu mimi ni kumuoa mtu ambaye ninampenda,” alisema Manaiki.
Hivi karibuni Manaiki alitangaza nia ya kumuoa Walper ambapo wazazi wake walimkatalia na kumwambia atafute msichana wa kutoka mkoa wake.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

IYOBO ASHIKWA NA KIGUGUMIZI KUHUSU MUME WA AUNT


DANSA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ameshikwa na kigugumizi kuhusu tuhuma za kumpachika mimba Aunt ambaye ni mke wa mtu.
 
Dansa wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo akiwa na Aunt Ezekiel.
Mose alionesha kigugumizi hicho baada ya kutaitiwa na paparazi wetu akiulizwa anajisikiaje kumpachika mimba mke wa mtu na vipi kama mume wa Aunt anayedaiwa kufungwa huko Dubai ataachiwa huru na kurudi.“Aaahhaa.. Mhh..Hayoo ni ya Aunt mwenyewe mimi hayanihusu,” alisema Mose kisha kimya kirefu kikafuatia kabla ya kuikata simu yake.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

PENINA KUPIGWA NDOA MUDA WOWOTE


MUIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Jennifer Raymond ‘Penina’, amefunguka kuwa anatarajia kufunga ndoa muda wowote kuanzia sasa.
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Jennifer Raymond ‘Penina’.
Akizungumza na Uwazi, Penina alisema kuwa harakati za kuolewa zipo jikoni hivyo anamuomba Mungu kile ambacho kinatarajia kufanyika kiweze kwenda kama alivyopanga ingawa hakutaka kumweka wazi mwanaume huyo kwa madai kuwa hataki kuibiwa.
“Mambo ya ndoa yapo tayari na anayesubiriwa ni mwanaume ambaye anataka kunioa ili alete barua ya uchumba, kwa sasa yuko nje kwa ajili ya mambo yake binafsi lakini atakapotua tu Bongo, muda wowote ndoa itafungwa,” alisema.
 USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Le Projectii:Wema Sasa Ampikia na Kumpakulia Ommy Dimpoz

Wakati mwanamziki wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz akiendelea kupepesa macho na kutikisa masikio kukanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwingizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ukaribu wao bado unatia mashaka na kuendeleza sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wapambe wao.

Japo kuwa Ommy alielezakuwa yeye na Wema ni marafiki toka kitambo kabla hata ya wema kuwa na mahusiano na mwanamziki Diamond, lakini  hii imezidiii.

Mbali na kuonekana wawili hawa kuwa pamoja sehemu mablimbali za starehe toka Ommy atoke Marekani, hili la kupikiwa na kupakuliwa nyumbani kwa Wema ndio limezidi kuchochea hisia kuwa wawili hao wanamahusiano zaidi ya USHKAJI.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwanadada Wema ambae na folloers zaidi ya laki nne , alibandika picha hiyo hapo juu akionekana kumpakulia chakula ambacho alijisifia ni kizuri na amekipika mwenyewe na kumtania Ommy kuwa alikuwa analeta pozi kwenye kula.

“Dat moment anapokuja home and umepika chakula alafu analeta pozi at first then unashangaa anaenda sahani mbili.... Talk About Good Food Made Real Good”- Wema aliandika mara baada ya kutupia picha hiyo.

Japo kuwa hadi sasa mwanadada Wema Sepetu ajajitokeza kukataa au kukubali juu ya yeye kuwa na mahusiano na Ommy lakini idadi kubwa ya wampambe wake mitandaoni na ifagilia sana hii “Couple”.

Tuvute subraaa.

Mzee wa Ubuyu
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Mrembo wa Nguvu Jokate Atupia picha zake Mpya za Kumtoa Nyoka Pangoni

 Mrembo Jokate Ameshare nasi Picha zake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram ..
Toa Maksi zako out of 10

 
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Jibu la Amber Baada ya Kanye West kusema alibidi aoge mara 30 ili kuwa na Kim Kardashian baada ya kuwa na Amber Rose.

Kwenye mahojiano na kipindi cha ‘BreakFast Club’ Kanye West alimkejeli mpenzi wake wa zamani Amber Rose kwa kusema alibidi aoge mara 30 baada ya kuwa naye ili Kim kardashian awe naye.

Kanye West alisema “Kim k angekubali kuwa na mimi kabla ya Amber basi nisinge kuwa na Amber Kabisa, ni ngumu kwa mwanamke kuwa na mwanaume aliyewahi kuwa na mahusiano na Amber, nilibidi nioge mara 30 ili Kim K anikubali”.

Amber amejibu kupitia twitter yake nakusema …



USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

PICHA: Uwoya aonyesha Tatoo yake ili watu waisome?

Vijimambo: Picha hii ya mrembo na mwigizaji  wa filamu anaezimikiwa na mashabiki wengi, Irene Uwoya imewaacha midomo wazi mashabiki wake huku wakiwa na alamaza kujiuliza vichwani mwao.

Irene aliibandika picha hii  mtandaoni bila kuandika kitu chochote kwahiyo ikawa kawa amewaachia fursa mashabiki wake watiririke.

Mbali na watu kusifia uzuri wake kwa ujumla, watu wengi walijikita kwenye tattoo yake ambayo amejichora juu ya kifua, karivu kabisa na shingo yake.

Wengi walijiongeza kuwa mwanadada huyu ameionyesha tattoo hiyo ili watu waweze kusoma ni nini alichokiandika, na wapo walio jaribu kuandika kile kilichoandikwa hapo.

Kiukweli mimi macho yangu hayako vizuri, mwenye macho tunaomba umtusidie, ameandika nini hapo?.

Mzee wa Ubuyu
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Mnaniboa Sana Mnaotoa R.I.P Kwenye INSTAGRAM Alafu Hamtokei Msibani -Shamsa Ford

"Morning my people..samahani kama nitakuwa nawakwaza but sometimes ni bora kutoa dukuduku lako..To be honest huwa wananiboa wale wa R.I.P WA INSTA...inaeleweka kwamba kutokana na majukumu ya kimaisha si kila kitu utaudhulia.sometimes inaweza ikatokea msiba labda umesafiri au unaumwa au dhalula yoyote inaeleweka
But hawa wenzangu na mimi msiba unatokea utaona R.I.P kubwa na kwenye msiba haendi..na si kwamba kabanwa wala,maana baadaye mnaweza kutana viwanja.isingekuwepo INSTA je.? Weka R.I.P na kama hujabanwa nenda msibani.nawajua hawa maana insta ataweka hadi vialama vya kulia but msibani halitokei ila usiku unakutana nalo club."
Unazungumzaije hili?
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Flora Mvungi: Bongo Movie Hatuna Ushirikiano Hata Kidogo

Mwigizaji wa filamu  ambae ameingia kwenye bongo fleva, Flora Mvungi ‘H.Mama’ amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa bongo movie hawapendani ndiomaana wanashindwa kufika mbali kisanaa.

Akinukuliwa na Gazeti moja la burudani, Flora alisema “Tukitaka kufanikiwa lazima sote letu liwe moja ili tufanye kitu kizuri,siku zote umoja ni nguvu cha msingi tukiamua kufanya kazi tusiangalie huyu bado msanii chipukizi siwezi kufanya naye kazi wote tushirikiane ili tufanye vitu bora na kupige hatua”.

Aliendelea kusema kuwa wasanii ambao tayari wamesha kuwa mastaa wakitafutwa ili afanye naye kazi lazima atataka malipo makubwa na ukiangalia bado chipukizi basi ndio mwanzo wa kakata tamaa.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Sifa za Mwanaume Amtakae Lady Jay Dee Kwa Sasa ....

Mwanaume mwenye vigezo gani ungependa kuwa nae kwa sasa?

JIBU :Anaejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma, anaeweza ku take care of me financially.Asiechepuka hovyo (Milupo kila kona ),Asiwe tegemezi.Hata kama sio tajiri lakini asinitegemee.Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar,Wala kulala nje kwa machangu wa Kinondoni au popote pale.Nikikohoa tu awepo hapo..

Kwa mtazamo wako anaweza kupata Mwanaume asiye na mapungufu?
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Msanii wa Vichekesho Atia Aibu Dodoma, Nyeti zake Zaonekana Wazi Akiwa Jukwaani

Mchekeshaji maarufu hapa Tanzani Masai nyotambafu ambaye kwa sasa na Presenter wa Star Tv kwenye kipindi cha MINI BUZZ Ambapo kwa sasa wapo Dodoma kw ajili ya maandalizi ya vipindi vyao ambavyo vinaruka kila siu kupitia luninga hiyo... Siku ya jana Masai aliibuka ndani ya kiwanja cha matei lounge na kufanya bonge la show ambapo hakifanikiwa kumaliza show kutoka na mbwembwe zake kumpoza..
Kwenye picha hapo tazama suruali aliyovaa hapo ni Model halafu anaenda kupiga msamba wewe unadhani kitatokea nini hapo?? Hapo ndipo alipobugi step Gafla tulisika Chaaaaaa........ Masamba alioupiga ulifanya aishiwe pozi na kutulia kama dadkika kadhaa akiwa hajui cha kufanya lakini alifanikiwa kujiogeza na kuvuta miguu yake na kujizogeza mpaka nyuma ya kibanda na kusimama huku akiwa amebana miguu na kuanza kutembea robo hatua... Ila tuligundua kwamba Msanii huyo alikuwa hajavaa nguo ya ndani na kuhofia nyeti zake kuonekana... Kiukweli masai alikuwa kwenye wakati mgumu sana mpaka mijasho kumtoka mwili mzima na badae alifanikiwa kutoka eneo hilo na kwenda kuvaa nguo ya ndani pamoja na suruali..tukio hilo lilitokea Matei Lounge Dodoma
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

ODAMA AFUNGUKA KUCHANGIA WANAUME!

MAMBO yanazidi kunoga ndani ya safu hii ya Sindano 5 za moto, kutokana na maombi yenu, leo tumemleta kwenu mwigizaji Jeniffer Kyaka ‘Odama’, tiririka naye:
 
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jeniffer Kyaka ‘Odama’.
Paparazi: Mambo vipi Odama! Tuanze moja kwa moja na swali la kwanza, hivi kwa sasa una mpenzi? Mbona hatumjui?Odama: Mambo poa! Mpenzi ninaye, nampenda muda bado wa kumuanika.Paparazi: Ulishawahi kuchangia bwana na mwanamke mwingine katika maisha yako?
Odama: Hapana, sina kumbukumbu hiyo.
Paparazi: Hadi leo hii unaweza kukumbuka idadi ya wanaume ambao umewahi kutoka nao kimapenzi?
Odama: Nakumbuka, kama mtu hukumbuki idadi basi lazima utakuwa una kichaa. Nakumbuka kwa sababu idadi ni ndogo, ila hapa sitataja idadi yao.
Paparazi: Hivi baba mtoto wako ni nani hasa au ndiye uliyenaye hadi sasa?
Odama: Hilo liweke kapuni kwa sasa, nitalizungumza ‘next time’.Paparazi: Inasemekana wewe ni miongoni mwa warembo ambao wanaoongoza kwa kutongozwa Bongo Movies, ni kweli?
Odama: Hiyo kawaida kwa mtoto wa kike, nadhani sipo peke yangu.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

JACK PENTEZEL: SITAKI TENA NDOA!

BAADA ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, Gadna Dibibi, mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ ameamua kufunguka na kuweka wazi kuwa hayuko tayari kuolewa tena.
 
Mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’.
Jack alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha yake hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake.
“Katika ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi kusema ndoa ni chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike kwanza sitaki tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena upya,” alisema Jack.
Jack alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa talaka hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika mapenzi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top