Moja kati ya makundi ya muziki ambayo yalitikisa ulimwengu wa tasnia hiyo kwneye miondoko ya Pop na Hip-Hop Blackeyed Peas limekuwa kimya kwa muda mrefu huku kazi ambazo zimekuwa zikisikika kutokana na watu wanaohusika na kundi hilo zikiwahusu kinara na Producer wa kundi Will-i-am na mwanadada Fergie.
Taarifa njema kwa wapenzi wa kundi hili ni kwamba kuna mpango wa kurudi kwa kundi hili baada ya kimya cha muda mrefu ambacho kilikuwa na maswali mengi huku wengi wakiamini kuwa kundi hilo limevunjika .
Kundi hilo limekuwa studio kwa muda mrefu sasa likirekodi albamu ambayo nit ole la pili la albamu ya mwaka 2010 iliyoitwa The Beginning na baada ya hapo kuna mpango wa kufanya Tour ya pamoja ambayo itakuwa kusherehekea kurdi upya kwa kundi hilo .
Kundi la The Blackeyed Peas linatarajia kurudi kwneye anga la muziki miezi michache ijayo.
Will-I-Am ambaye miezi michache iliyopita alikanusha taarifa za blackeyed peas kurudi upya alisema kuwa kundi hilo limekuwa studio kwa zaidi ya miezi miwili na kila mmoja kati ya wanakundi amekuwa na furaha huku kukiwa na msisimko mkubwa kuelekea hatua inayofuata .
Kundi hilo linatengeneza Albamu mpya na pia litafanya ziara ya kuadhimisha miaka 20 ya kundi hilo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment