Siku si nyingi kuanzia sasa klabu ya Barcelona itakuwa na uongozi mpya ambao utaingia madarakani kuelekea mwishoni mwa msimu huu wakati ambapo klabu hii itafanya uchaguzi wake mkuu .
Hii ni baada ya Rais Jose Maria Bartomeu kutangaza kuwa klabu hii itafanya uchaguzi wake mwaka huu akisogeza mbele uchaguzi huo ambao awali ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka 2016.
Hii ni kutokana na shinikizo kubwa ambalo amepata toka kwa wanachama wa klabu hiyo ambao wanafahamu kiini cha migogoro inayoendelea sasa kuwa uongozi mbovu uliokuwepo kwenye klabu hiyo chini ya rais wa awali Sandro Rosell ambaye alijiuzulu mwaka jana.
Moja kati ya majina mabayo yamekuwa yakitajwa kuhusika na uongozi mpya ni rais wa zamani Joan Laporta ambaye amekuwa akisema wazi kuwa anataka kurudi kuongoza klabu hiyo .
Rais wa zamani Joan Laporta ana mpango wa kurudi kwenye klabu hiyo .
Pamoja na hayo bado Laporta anapewa nafasi kubwa ya kuchukua kiti cha urais endapo atatangaza kugombea.
Tayari Laporta ameshaweka mipango ya uongozi mpya wa timu hiyo kuanzia kwenye benchi la ufundi ambako amezungumza na kocha wa zamani wa Barca Pep Guardiola ambaye amekubali kimsingi kurejea Barca katika nafasi ya Ukurgenzi wa Ufundi mara mkataba wake na Bayern Munich utakapomalizika .
Laporta ana mpango wa kumrudisha kocha wa zamani Pep Guardiola kama mkurugenzi wa ufundi.
Chini ya Laporta nahodha wa sasa Xavi Hernandez atateuliwa kuwa kocha mpya baada ya kustaafu
kucheza soka.
Nahodha wa zamani Carles Puyol na Eric Abidal wataunda sehemu ya benchi la ufundi chini ya Xavi
Hernandez wakiwa wasaidizi wake.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment