‘Die hard fans’ wanaweza kufanya lolote
kuhakikisha wanampa ushindi msanii wao katika shindano lolote
linalohiotaji ushiriki wao hasa wa kupiga kura au maoni, kama
kinachofanywa hivi sasa na mashabiki wa Diamond Platnumz katika tuzo za BET.
BET wanaendelea kuweka majina ya nominees katika page zao za mitandao ya kijamii ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuwaongezea ushawishi wa kupewa ushindi wasanii
wao. Kama ilivyokuwa jana picha ya Diamond imeendelea kupata likes na
comments nyingi katika Facebook ya BET, mpaka sasa ina likes 2649 na
comments 5471 huku Davido akiwa na likes 1465 na comments 619 tu.
Upande wa Instagram ya BET Awards picha ya Diamond iliyowekwa jana usiku na maelezo haya:
‘Dbl tap this pic if you want #DiamondPlatnumz to win #BestInternationalAct: Africa @ the #BETAwards this yr’,
Hadi sasa ina likes 3275 na comments
4354 huku picha ya Davido katika akaunti hiyo ya IG ya BET iliyowekwa
siku mbili zilizopita ina likes 518 na comments241 tu.
Cha kushangaza mashabiki wa Diamond
wameamua kutoka nje ya kile kinachotarajiwa baada ya kuamua ku-comment
jina la Diamond katika picha hiyo ya Davido.
Post a Comment