STAA Jacqueline
Wolper Massawe, ambaye ni muigizaji mahiri wa filamu, amewapiku nyota
wenzake wa tasnia hiyo baada ya kufanya kumbukumbu ya siku yake ya
kuzaliwa Jumamosi iliyopita kwa namna tofauti kabisa, kwani badala ya
kuita marafiki kwenye pati kubwa inayoambatana na vyakula na vinywaji,
yeye alikwenda kuwatembelea wazee wanaolelewa katika Kanisa Katoliki la
Msimbazi, jijini Dar.
Staa wa filamu Bongo Jacqueline Wolper Massawe akisalimiana na Sista wa Kanisa Katoliki la Msimbazi, jijini Dar.
Katika kituo hicho kinachowalea wazee wa
kike na kiume, Wolper aliyeambatana na rafiki yake Kajala Masanja na
wale aliowatambulisha kama Wolper Family, muigizaji huyo alitoa zawadi
ya mchele mifuko miwili ya kilo 50 kila moja, sukari mifuko miwili ya
kilo 50, sembe kilo 50 pia, sambamba na mafuta ya kupikia madumu mawili,
vitu ambavyo alikataa kutaja thamani yake.
Wolper Massawe akitoa zawadi katika kituo cha kulelea wazee cha Kanisa Katoliki cha Msimbazi.
“Siku hizi nimekuwa mtu mzima,
nimeachana na mambo ya sherehe kwa sababu nimeona ninakuwa napoteza pesa
kwa mambo yasiyo ya muhimu, ni jambo la heri kwangu kuwasaidia wazee
kwani nawapenda na naamini hata wao wanatupa sapoti kubwa sana kwenye
kazi zetu, japo kuna watu walitarajia waone nini kitafanyika kwenye siku
yangu hii ya kuzaliwa kuhusu sherehe,”alisema Wolper.
Wazee wakimshukuru Wolper Massawe kwa upendo aliouonyesha kwao.
Marafiki zake kutoka Wolper Family
walisema ni wao ndiyo waliomshauri staa huyo kufanya kitu hicho ili kuwa
tofauti na wenzake ambao kumbukumbu ya kuzaliwa kwao hufanywa kwa
matumizi makubwa ya fedha yasiyo ya lazima.
Wolper akipozi pichani na shosti yake Kajala.
“Alitaka kufanya sherehe tukamshauri
aachane na hilo suala tuliona atapoteza pesa kwa sababu angefanya
sherehe watu wangekunywa pombe, wangevaa vinguo vya ajabu, kitu ambacho
ni kama laana kwake, badala yake kwa hili alilolifanya atapata baraka na
mambo yake yatamnyookea,” alisema mmoja wa mashabiki wake kutoka Wolper
Family.
Baada ya kukabidhi msaada wa vyakula
hivyo, mmoja wa wazee hao Bibi Rachel Christopher, alimpa somo Wolper
kuwa ni vema wakaishi vizuri na mashabiki wao na kuachana na mavazi ya
ajabu kwani yanawashushia hadhi zao.
Wolper akiwa katika picha ya pamoja na Wolper Family.
“Mimi huwa naangalia sana filamu zao,
ninawapenda na huyu leo katimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake,
tunamuombea uzima, afya tele na maisha marefu,” alisema bibi huyo ambaye
pia aliwataka waigizaji wa kiume na wasanii kuacha kuvaa suruali kwa
mtindo wa kata K.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment