Haya ni majeraha yanayotokana na shambulizi alilopokea mwananchi huyu kutoka kwa askari Magereza wa Gereza la Shinyanga
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa kijiji cha Nhelegani manispaa ya
Shinyanga ameshambuliwa kwa kipigo na askari wa Jeshi la Magereza na
kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kugoma kuwapa
askari hao soda na biskuti.
Tukio
hilo la aina yake limetokea katika Gereza la wilaya ya Shinyanga wakati
mwananchi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Lugenzi Maguta (45)
alipokwenda kumsalimia ndugu yake aliyeko mahabusu aliyemtaja kwa jina
la Mahushi Nangale.
Mbali
ya kushambuliwa kwa kipigo hadi kupasuka katika miguu yake yote miwili
kutokana na kupigwa virungu bado askari magereza hao wanadaiwa kumgeuzia
kibao kwa kumfungulia shitaka la kufanya fujo gerezani tuhuma ambazo
alidai ni za uongo kwa vile hakuna fujo yoyote iliyotokea.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya
serikali ya mkoa wa Shinyanga, Maguta alisema askari waliomshambulia
waliokuwa wamevaa kiraia hawakuwa zamu bali walikuwa nje ya gereza
waliamua kumshambulia kwa madai walichukizwa na kitendo chake cha
kukataa kuacha soda na biskuti alizokuwa nazo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment