Kitandani mtoto wa kike nilijituma kwa kumgusa hapa na pale kuhakikisha mzee kalilia mkononi au mdomoni. Sikuishia hapo mtoto wa kike katika kukatana kiu nilijituma huku sifa zote nikimpa yeye kuwa hakuna mwanaume anayejua mapenzi kama yeye.
Huku nikijituma, mpira wa kona wangu, golikiki yangu, kurusha mimi, kukaba mimi, kushambulia mimi.
Mambo yote yalimfanya azidi kunishangaa na alijiuliza nilikuwa wapi siku zote, sasa hebu ona baada ya mpambano mzee mzima akihema kama bata aliyedondoka kwenye mnazi, nilikaa upenuni mwa kitanda na kuangua kilio. Mzee mzima kachanganyikiwa kulikoni.
Hapo ndipo lilipoanza kulalamika kuwa siku hizi hanipendi na kuonekana halifurahii penzi langu wakati huo nikijua kabisa nimempeleka puta na kumchanganya na penzi nililompa.
Mzee wa watu alijiapiza kutekeleza siku ya pili, na kweli siku ya pili vitu viliteremka vya kumalizia nyumba. Hiyo ilikuwa kwangu sasa nasema na wewe ambaye ulikuwa ukifanya ili kumkomoa mumeo au mpenzio. Ni makosa kufungua mahakama kitandani, unapoteza maana ya kitanda hasa mkiwa katika hali ya kuburudishana.
Kama una lako linalokukera jitume hasa kimapenzi ili kumfanya mpenzi au mumeo ajue nini umuhimu wako kwake. Jitume huku akimpa sifa ambazo ni haki yake kitu kitakachompa kichwa. Uoneshe uanamke wako hata baada ya kumkata kiu bila kinyongo hata ukiomba ukitakacho utapewa, si kutumia njia ya mkato kutatua tatizo lako.
Kufanya hivyo ni kutupa nafasi tuwachukue wanaume zenu kwa urahisi. Zinduka, mwanamke mwenzangu usimbanie mumeo, jitume ili ukitakacho ukipate kwa urahisi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment