Baadhi ya wadau wakiwa kwenye zulia jekundu ‘red carpet’ wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Muigizaji
mkongwe, Mzee Chillo (kushoto), mwandishi wa kitabu Emmanuel
Zirimwabagabo, mama yake Kanumba na Waziri Mahanga wakiwa kwenye pozi la
pamoja.
Muigizaji Rose Ndauka (kulia) akiwa na mdau wakiwa na kitabu cha Kanumba.
Waigizaji walioibuliwa na marehemu Kanumba, Jenipher na Patrick wakiwa pamoja.
Waziri Mahanga (kushoto) akizindua kitabu na mwandishi Emmanuel.
Mzee Chillo (kushoto) akiteta jambo na Emmanuel.
Mwanamuziki Christian Bella (kulia) akitumbuiza na Malaika Band.

Wadau wakicheza muziki.
Mama Kanumba (kushoto)akisalimiana na mwanamuziki Stara Thomas.
…Akimkumbatia muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu'.
Muigizaji Mayasa Mrisho (kushoto) akiwa na Rose Ndauka.
NAIBU Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga, jana amezindua rasmi kitabu cha marehemu Steven
Charles Kanumba, Kinachoitwa ''Steven
Charles Kanumba: The Great Fallen Tree'' kilichoandikwa na Emmanuel Zirimwabagabo, raia wa Congo anayeishi nchini Canada.
Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo alisema vijana
wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi
kwa nguvu kama marehemu Kanumba na si kulalamika kila siku, jambo
linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na
mengineyo.
Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika
kukinunua kitabu hicho cha Kanumba, ambacho pia amekiandika kwa lugha
ya Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kukisambaza dunia nzima.
Alisisitiza kwamba vizazi vijavyo ambavyo havikumuona vitamfahamu
muigizaji huyo nguli wa Tanzania kupitia kitabu hicho kilichozungumzia
maisha yake yote ya enzi za uhai.
(Na Gabriel Ng'osha/GPL).
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment