
Mwenyekiti
wa Kamati Kuu ya CCM, Jakaya Kikwete akipiga makofi wakati alipowasili
katika mkutano wa chama hicho Mjini Dodoma hivi karibuni.
Dar
na Z’bar. Vikao vya Kamati Kuu ya CCM na Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar
vinaonekana kuwa huenda vikaiweka hadharani siri nzito za urais wa
Jamhuri ya Muungano.
Mkutano
wa sekretarieti ndiyo utakaoanza leo ukifuatiwa na Kamati Maalumu ya
NEC Zanzibar huku Kamati Kuu ya CCM ikitarajiwa kukutana Jumanne wiki
ijayo katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kujadili na kutathmini hali ya
kisasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Kikao
hicho kimekuja huku wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kupitia chama hicho wakipishana kwa usafiri wa ndege na boti
kwenda Zanzibar kutafutwa kuungwa mkono na wajumbe wa NEC na waliopo
visiwani humo.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alithibitisha kikao hicho
kufanyika Zanzibar na kitaoongozwa na Mwenyekiti wake Rais Dk Jakaya
Kikwete ambaye amebakisha muda mfupi kumaliza muhula wake wa uongozi
tangu aingie madarakani mwaka 2005.
Vuai alisema Kamati Kuu ya CCM itakutana, itatanguliwa na Kikao cha Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar.
Alisema
suala kubwa ambalo watalijadili ni kuangalia mwenendo wa utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 tangu kumalizika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2010.
Hata
hivyo, Vuai alisema hayuko tayari kuzungumzia ajenda ya kikao cha
Kamati Kuu kwa vile majukumu hayo yako kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi
Taifa, Nape Nnauye.
Pia,
alisema Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar itakuwa na ajenda ya mengineyo
itakayojadili hali ya kisiasa tangu kumalizika uchaguzi mkuu uliopita
ambapo kikao hicho tayari matayarisho yake yamekamilika kabla ya kuanza
kamati Kuu kukutana visiwani humu.
Nape
Hata
hivyo, Nape alisema jana kuwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM,
inakutana leo jijini Dar es Salaam kupanga ajenda zitakazojadiliwa
kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho
itakayokutana Zanzibar Jumanne ijayo.
Alisema kuwa kikao hicho ni cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.
Kikao
cha Kamati Kuu kinakutana na kukiwa na patashika ya makada wa CCM
wanaotajwa kuwania nafasi ya urais wakipishana kwa safari za usafiri wa
majini na angani na wapambe wao kukutana na wajumbe wa NEC na mkutano
mkuu katika vikao vya faragha Pemba na Unguja kuomba ushawishi wa
kuungwa mkono.
Hali
ya kisiasa Zanzibar, inadaiwa kuchafuka na kuhatarisha uimara wa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) baada ya vigogo wa Serikali hiyo
kuanza kunyosheana vidole hadharani.
Inaelezwa
kuwa joto la uchaguzi wa urais ndilo ambalo limesabasisha hali hiyo
itokee. Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim, Seif Shariff Hamad na Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein huenda wakachuana katika uchaguzi wa
urais mwaka huu.
Sauala
lingine zito ambalo linaweza kujadiliwa katika vikao hivyo ni la kashfa
ya escrow ambayo imewakumba mawaziri na baadhi ya madaka wa chama
hicho.
ADVERTISEMENT
Mawaziri
ambao wamekumbwa na kashfa hiyo ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni Mjumbe
wa Kamati Kuu na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo.
Profesa
Tibaijuka tayari ameondolewa kwenye nafasi yake ya uwaziri baada ya
kupokea kiasi cha Sh1.6 bilioni kutoka kwa Mfanyabiashara maarufu
nchini, James Rugemarila ambaye ni mbia wa Kampuni ya Kufua Umeme ya
IPTL.
Mwingine
anayetajwa kuhusika ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew
Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, William
Ngeleja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Mbali
na wahusika wa Akaunti ya Escrow, vikao hivyo huenda vikajadili ripoti
ya maadili ya viongozi ikiwamo waliokumbwa zuio la kujihusisha na
kampeni za kuwania urais mapema kwa miezi 12, huku mienendo yao ya
kisiasa ikifuatiliwa.
Waliozuiwa
kufanya kampeni ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi, Teknolojia
January Makamba, Waziri Mkuu Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Wengine
ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na
aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa
Sengerema, William Ngeleja.
Hata
hivyo, Nape alipoulizwa kuhusiana na wagombea wa urais kufanya kampeni
za nguvu na wengine kutumia mitandao ya simu kusambaza ujumbe, alikataa
kuzungumza chochote kuhusiana na suala hilo pamoja na sakata la escrow
iwapo litapewa nafasi katika vikao hivyo vya chama.
Mtikisiko Zanzibar
Maalim
Seif hivi karibuni alikaririwa akisema atapambana na Rais wa Zanzibar,
Dk Ali Mohamed Shein kwenye vikao vya Serikali na kulalamika kuna baadhi
ya masheha, wakuu wa wilaya na mikoa wakiwanyima wananchi haki ya
kupata vitambulisho vya Uzanzibari mkaazi na kutoandikisha kwenye
Daftari la Kudumu la Kupiga
Akijibu
dai hilo, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Balozi Seif alisema hakuna
wananchi wanaokatazwa kupata Vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi na
kueleza kuwa chini ya Sheria Namba 7 ya mwaka 2005 hakuna mtu ambaye
anaweza kupewa kama siyo mkaazi wa Zanzibar kwa miaka mitatu.
Balozi
Seif alisema Serikali haitakubali kupata hasara ya kuzalisha
vitambulisho kutokana na idadi kubwa ya zaidi kuandikishwa watu ambao
siyo wakazi ya Pemba, wakati kuna vitambulisho vingi vimeshindwa
kuchukuliwa na wenyewe ambao alisema ni mamluki.
Mjumbe
mmoja wa NEC ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alithibitisha vigogo
wanaowania urais na wapambe wao kumshawishi kuingia katika kundi lao.
Wagombea urais
Vigogo
wa urais waliofanya ziara kwa nyakati tofauti hivi karibuni visiwani
Zanzibar ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano) Stephen Wasira, Mbunge wa Sengerema
William Ngeleja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye amealikwa kuhudhuria
Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) leo yaliyoandaliwa na Mbunge wa
Mpendae na Mafanyabiasha mashuhuri, Salum Turky.
Kadhalika Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye wakati wa Sikukuu ya Krismasi ya mwaka jana alikuwa Zanzibar.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment