Kocha
wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic akiongoza kikosi chake katika mazoezi
ya timu hiyo yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijao, mjini
Mtwara, wakijifua kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Ndanda.
Umati
wa mashabiki wakishuhudia mazoezi ya kikosi cha Simba jana kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona huko Mtwara, wakijiandaa na mchezo wa leo,
dhidi ya Ndanda.
Straika
mpya wa Simba, Simon Sserunkuma (wa kwanza kulia), akiwa na wezake
katika kunyoosha viungo kabla ya mtanange wa leo dhidi ya Ndanda.
Straika
Dan Sserunkuma katika harakati za kuwaziba mdomo wanaombeza kuwa
hajafanya kile mashabiki walichotegemea tangu ajiunge na Simba akitoka
Gor Mahia ya Kenya.
Kocha
wa Simba, Kopunovic ‘aki- control’ mpira katika mazoezi ya timu hiyo
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakijiandaa kuwavaa wenyeji wao,
Ndanda.
Hii
ndio Nangwanda Sijaona, uwanja ambao Azam waliodoka vichwa chini
mwanzoni mwa msimu huu, je, Simba watatoka? Jibu ni baadaye.
(PICHA: RICHARD BUKOS/GPL , MTWARA)
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment