Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mara limewakamata watu wanne na bunduki mbili
aina ya SMG na risasi 167 zilizokusudiwa kutumika kwa ujangili wa
Tembo katika hifadhi ya Serengeti
Silaha zilizokamatwa
Jeshi
la polisi mkoa wa Mara kwa kushirikiana na askari wa
hifadhi ya taifa ya serengeti limefanikiwa kukamata bunduki mbili
aina ya SMG na risasi 167 ambazo zilikusudiwa kutumiwa na watu
wanne wanaotuhumiwa kuhusika na vitendo vya ujangili wa
mauaji ya Tembo katika hifadhi hiyo ya taifa ya serengeti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishina msaidizi Philip Alex Kalangi, amesema kuwa polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi hiyo ya taifa walipata taarifa kuhusu majangili hao kuingia katika hifadhi hiyo ya taifa kwa lengo la kuua tembo kisha kuweka mtego ambao ulishtukiwa na majangili kabla ya kukimbia na kutelekeza bunduki hizo mbili, risasi 167 na meno mawili ya tembo.
Hata hivyo kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mara amesema katika operesheni ambayo inaendelea katika wilaya za Musoma, Bunda na Serengeti, askari wa jeshi la polisi wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu watano wanadaiwa kutumia funguo bandia huku wakivunja na kuiba katika ghala la kuhifadiwa bidhaa mbalimbali katika mtaa wa Serengeti mjini Musoma

USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment