Huenda kukawepo na hali ya kutokuelewana baina ya wachezaji wa Real Madrid baada ya kiungo mshambuliaji Gareth Bale kuzomewa na mashabiki wa klabu hiyo huku mwenzie Cristiano Ronaldo akionekana wazi kumlaumu mchezaji huyo kwenye mchezo kati ya Real Madrid na Espanyol uliopigwa jumamosi .
Gareth Bale ambaye kwenye mchezo huo alifunga bao moja kwa njia ya mpira wa adhabu ndogo huku akiwa na mchango wa kuanzisha shambulizi lililozaa bao la pili kwa timu hiyo alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu baada ya wenzie kumlaumu kwa kushindwa kumpa Ronaldo pasi.
Picha za Televisheni zilimuonyesha Ronaldo akitamka neno la tusi kumuelekea Bale kutokana na kitendo hicho hali ambayo inaashiria kutokuwepo kwa maelewano miongoni mwa mabingwa hawa wa ulaya .
Ronaldo akionyesha kukerwa baada ya mwenzie Gareth Bale kushindwa kumpa pasi akiwa kwenye
nafasi ya wazi ya kufunga .
Gareth
Bale akiwa mnyonge baada ya kuzomewa na mashabiki wa Real Madrid
kufuatia kushindwa
kumpa Ronaldo pasi kwenye mechi dhidi ya Espanyol.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment