
Mshambuliaji
wa Simba SC, Danny Sserunkuma akiwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar wakati
wa mechi ya fainali Kombe la Mapinduzi usiku huu huko Zanzibar.
Patashika wakati wa mtanange huo.
Ramadhan Singano 'Messi' akijaribu kumtoka beki wa Mtibwa, David Luhende.

Mashabiki wakifuatilia mechi hiyo.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza mechi hiyo.
Kikosi cha Mtibwa Sugar kilichoanza mechi hiyo ya fainali.
KLABU ya Simba imetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa penalti 4-3
dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya matokeo ya 0-0 katika dakika 90, usiku
huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Penalti za mabingwa hao mara tatu wa Kombe la Mapinduzi ziliwekwa
kimiani na Awadh Juma, Hassan Kessy 'Danny Alves', Hassan Isihaka na Dan
Sserunkuma huku za Mtibwa Sugar zikifungwa na Ally Lundenga, Shabaan
Nditi na Ramadhan Kichuya.
Katika michuano hiyo, Simon Msuva wa Yanga ameibuka mfungaji bora
akiwa na mabao 4, Salim Mbonde wa Mtibwa akichukua tuzo ya mchezaji bora
huku kipa wa Mtibwa, Said Mohammed akiwa ndiye kipa bora wa michuano
hiyo iliyomalizika usiku huu.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL, ZANZIBAR)
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment