Mabingwa wa ulaya , Real Madrid wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwafunga wapinzani wao toka jijini Madrid Getafe katika mchezo wao wa 18 wa ligi kuu ya Hispania .
Madrid walihsinda mchezo huo kwa matokeo ya 3-0 wakifunga mabao yao kupitia kwa Cristiano Ronaldo na Gareth Bale ambapo Ronaldo alifunga mabao mawili .
Ushindi huu unawafanya Real wafikishe idadi ya pointi 45 baada ya kucheza michezo kumi na nane .
Mabao matatu dhidi ya Getafe yalifungw ana Ronaldo (2) na Gareth Bale (1)
Real Madrid bado wana mchezo mmoja mkononi ambao utawafanya wafikishe idadi ya michezo 19 kama ilivyo kwa timu nyingine za ligi ya Hispania .
Ronaldo anaongoza kwa kufunga magoli (28) na kwenye pasi za mwisho (9).
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment