Pili ni maneno makali yaliyoupasua moyo wake baada ya kuitwa mkimbizi na kukumbushiwa vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Burundi.
“Haukuwa mpira, hauwezi kuamini kama kweli wale walikuja uwanjani kucheza soka. Walinipiga kiwiko, wakanipiga ngumi na mwisho Michael alinikaba shingoni zaidi ya mara moja na kunifanya nishindwe kupumua.
Osei wa Ruvu akizikunja na Tambwe.
“Hii ni hatari, kuna mtu anaweza kuanguka akapoteza maisha siku moja.
Wale wanajeshi hawaingii uwanjani kucheza soka, wanakwenda kucheza na
mwili wa wachezaji wenzao.“Ila nilishangazwa na mwamuzi kutoa kadi kwetu huku akionekana kuwahofia wanajeshi. Ukimwambia mwamuzi anachekacheka tu, sijui alikuwa anamaanisha nini.
Osei wa Ruvu akimzuia Tambwe asipelekea madhara langoni mwako.
“Nafikisha hata mashitaka kwa TFF, wawaangalie waamuzi na
kuwasisitiza wafanye kazi yao kwa haki na kuwalinda wachezaji
waliokwenda kucheza soka na si ugomvi,” alisema Tambwe na kuongeza.“Kilichoniuma zaidi ni matusi na kuitwa mkimbizi, tena wakisema nimekimbia vita Burundi. Nimevumilia sana, ajabu wale ni askari lakini hawaonyeshi kuwa wanajua athari za vita.
“Vita Burundi, pia inaweza kutokea hapa. Hakuna anayetaka mabaya kama hayo, kumwambia mtu haujui kapoteza ndugu au vipi, si sahihi. Uliona Zidane alimpiga (Marco) Materazzi,” alisema kwa sauti ya taratibu.
“Sijalala, daktari wa timu aliniandikia dawa ya maji, nikaweka jichoni na pia ya kunywa. Bado jicho halioni vizuri.
“Sijawahi kutamka hata siku moja, lakini leo ninatamka kuwa soka la hapa nchini hivi sasa ni vita na siyo burudani tena, haiwezekani mchezaji anacheza soka huku akirusha ngumi, viwiko na mateke uwanjani huku mwamuzi akiangalia tu bila ya kutoa maamuzi yoyote.
“Pia ninamshangaa huyu jezi namba 4 (George Osei), yeye kila ninapokutana naye lazima acheze kwa kunipania kwa kunichezea rafu za makusudi, kunirushia ngumi na viwiko, sasa angalia kama leo kanipasua mdomoni na jicho linaanza kuvimba, hapa ninapoongea na wewe nashindwa kuona mbele vizuri,” alisema Tambwe kwa masikitiko makubwa na kuomba TFF kuchukua hatua zinazostahili kwa mchezaji huyo ili kurejeshe nidhamu mpirani.
(PICHA: GPL)
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment