Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

ASKARI WANANE WA IRAQ WAUAWA KWA KUWAPELELEZA ISIS

Mateka wakiwa wamepigishwa magoti tayari kwa kuuawa.
Mateka wakipelekwa sehemu ya kuadhibiwa kwa ujasusi dhidi ya ISIS.
Baadhi ya wanajeshi wa usalama wa ISIS wakionyesha bastola zao. 
Namna ambayo wapiganaji wa ISIS huvaa nguo zao.
WAPIGANAJI wa Taifa la Kiislam (ISIS) lililoanzishwa katika maeneo ya Syria na Iraq, wametoa picha za maofisa wanane wa polisi wa Iraq waliokamatwa na kuuawa kwa kufanya ujasusi dhidi ya ISIS kwa ajili ya serikali ya Iraq.
Kwa mujibu wa habari kutoka Taifa la Kiislam, kiongozi wa watu hao alitajwa kama Kepteni Hossam Salah Bnosh ambapo yeye na wenzake walibadili madhehebu yao na kujiunga na madhehebu ya Kiislam ya Sunni, lakini baadaye wakachukua fursa hiyo kufanya ujasusi dhidi ya ISIS.
Mauaji hayo ambayo yalifanyika mchana, yalikuwa na lengo la kuwaonyesha walimwengu adhabu hiyo iliyotolewa kwa watu hao ambao walikuwa wamevishwa ‘magwanda’ ya rangi ya chungwa kama wavaayo wafungwa wa gereza la Guantano linalomilikiwa na Marekani huko Cuba.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top