Miss
Tanzania 2013/14, Happiness Watimanywa akiwashukuru watanzabia kupitia
kikao chake na waandishi wa Habari kilichofanyika mapema leo katika
Ukumbi wa Habari Maelezo Posta jijini Dar es Salaam.
Miss
namba mbili 2014/15 Jihan Dimack (kushoto), akiwa na Happiness
Watimanywa wakati alipokuwa akiwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura
katika Ukumbi wa Habari Maelezo Posta jijini Dar es Salaam.
MISS Tanzania /World 2014, Happiness
Watimanywa mapema leo amewashukuru watanzani wote waliyotumia muda wao
kumpigia kura alipokuwa katika harakati za kuiwakilisha nchi katika
kuwania taji la kuwa Miss World 2014.
Akizungumza kwenye kikao cha waandishi wa
habari kilichofanyika ndani ya Ukumbi wa Habari Maelezo Posta jijini Dar
es Salaam, alisema kuwa alipokuwa katika mchakato huo alifarijika sana
baada ya kujikuta akiingia kwenye nafasi ya pili ya Dunia, mashindano
hayo kupitia kitengo cha kura za watu.
“Sina budi ya kutumia muda huu kuwashukuru
Watanzania wote kwa mchango wao waliouonyesha kwangu, maana katika
nafasi ya kura ya kuchaguliwa na watu kupitia mitandao nilishika nafasi
ya pili jambo ambalo lilinipa faraja kubwa sana na kunifanya niione nchi
yetu ni namna gani ilivyoamka katika suala zima la kuwajali watu wake,”
“Kwakutambua hilo napenda kutoa shukurani
zangu kwa kila mtanzania aliyetumia muda wake kunipigia kura hata
waliyoniombea, naamini kabisa kwa namna walivyonifanyia siku nyingine
kama kuna mrembo atakaye enda huku atakuwa nanafasi kubwa sana ya kutwaa
taji hilo,” alisema Timanywa.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment