DAH MASIKINI! Hivi
ndivyo unavyoweza kusema wakati unapomuona msanii wa muziki wa kizazi
kipya, Cheka Hija, maarufu kama Bi. Cheka kutoka Kundi la Mkubwa na
Wanawe, linaloongozwa na Said Fella ‘Mkubwa’ lenye maskani yake, Temeke
jijini Dar es Salaam.
Mtoa habari wetu aliwasiliana na gazeti
hili na kulieleza kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 55, hivi
karibuni alianguka ghafla nyumbani kwake na kukata kauli, wakati
alipokuwa akienda chooni kujisaidia.
Wikiendi iliyopita, Amani lilifika
nyumbani kwa msanii huyo mzee, anayeishi Bunju B, nje kidogo ya jiji la
Dar na kumkuta akiwa na wajukuu zake huku hali yake ikiwa tete tokea
alipoanguka Oktoba mwaka huu.
Akiwa anaishi katika kijumba chake kilichojengwa kwa miti na kukandikwa udongo, mtu anayemuona katika luninga akifanya vitu vyake, asingeweza kuamini kama hapo ndipo anapoishi.
Akiwa anaishi katika kijumba chake kilichojengwa kwa miti na kukandikwa udongo, mtu anayemuona katika luninga akifanya vitu vyake, asingeweza kuamini kama hapo ndipo anapoishi.
Upande wa nyumba yake.
“Ukweli nilikuwa na hali mbaya, afadhali
sasa, naongea na kusimama kwani nilikuwa siwezi kutembea, wiki
iliyopita alikuja meneja wetu, Yusuf Chambuso na akina Dogo Aslay.
“Jamani maisha yangu kwa sasa ni magumu
kwani siwezi kufanya kazi yoyote na sina msaada na kwenye muziki sijaona
faida yoyote labda ya nguo tu, kwamba nilizoea kuvaa madela na kanzu
sasa nina suruali,” alisema Bi Cheka kwa machungu.
Bi Cheka akiwa na wajukuu zake.
Alisema anasikitishwa na maisha yake
kwani kutokana na umaarufu wake, mtaani kwao anaonekana kama mtu mwenye
uwezo, wakati siyo kweli kwani anaishi kwenye nyumba ya tembe katikati
ya nyumba nzuri.
“Kuhusu malipo makubwa kuwahi kupata ni
shilingi laki tatu nilizolipwa kwenye shoo ya Fiesta mwaka juzi, hizo
ndizo hela kubwa niliyowahi kupata katika muziki.”Gazeti hili
lilimtafuta Fella ambaye alikiri Bi. Cheka kuumwa, akisema anasumbuliwa
na magonjwa ya uzee na kwamba ahadi yake ya kumsaidia kujenga nyumba
imeishia kwenye mchango wake wa matofari.
...Bi Cheka akiimba na Chege.
“Mimi kama Fella nimesaidia ninapoweza,
nimemchangia matofari kidogo, kwa hiyo watanzania wenzangu nao tuungane
tumchangie ili aweze kurekebisha kibanda chake,” alisema.
Global Publishers inaanzisha kampeni
maalum ya kumsaidia na hivyo inawaomba watanzania kumchangia msanii huyu
ili apate nyumba nzuri na matibabu yake. Ili kumsaidia tuma fedha
kwenye namba 0654-880707 ambayo itasimamiwa na kampuni.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment