
Polisi wakiondoa vizuizi vilivyowekwa na wananchi barabarani.
Wananchi wakionekana kusikitishwa na kitendo cha polisi kuondoa vizuizi vyao barabarani.
Polisi wakiwa wamemweka chini ya ulinzi mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele kufunga barabara.
Wananchi wakitawanyika baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi.
WAKAZI wa
eneo la Kawe-Bondeni jijini Dar es Salaam jioni hii wameamua kukaa
katikati ya barabara eneo hilo wakiishinikiza serikali kuwawekewa matuta
wakidai kuchoshwa na ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikiondoa
uhai wa wapendwa wao wakiwemo wanafunzi.
Hata hivyo
malengo yao hayakuweza kutimia sawasawa baada ya polisi kuingilia kati
na kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Wananchi
hao wamefikia uamuzi huo baada ya kudaiwa fedha za kulipia gharama za
kuhifadhi mwili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mwili huo ni wa
mwananchi aliyegongwa na gari jana eneo hilo hilo linalolalamikiwa na
wakazi hao.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment