Wakati
kilele cha sikukuu ya Krismas kikikaribia Rais wa Marekani Obama na
familia yake walikua wakisherekea pamoja katika uzinduzi wa tamasha la
krismas lijulikanalo kama
Christmas in Washington Concert ambalo hufanyika kila mwaka.
Obama akiongozana na mkewe pamoja na watoto wake wawili Malia pamoja
na Sasha waliweza kusherekea tamasha hilo sambamba na watoto wengine
pamoja na watu maalum walioalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika
moja ya nyumba za makumbusho ya Taifa.
Likiwa ni tamasha la 33 kufanyika tangu kuanzishwa litapambwa na
wanamuzuki mashuhuri pamoja na watoa mada ambao watakua wakizungumzia
mambo mbalimbali yanayohusiana na sikukuu ya Krismas.
Lengo la tamasha hilo pia lililenga kusaidia mfumo wa Taifa wa huduma za afya kwa watoto.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment