WAKATI kila mtu akiamini mwalimu wake wa lugha ya
Kiingereza ni Wema Sepetu ‘Madam’ staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’ ameibuka na kudai aliyemfundisha lugha hiyo ni aliyekuwa
mpenzi wake, Peniel Mungilwa‘Diamond aliwataka watu wote waliokuwa
wakiamini Wema ndiye mwalimu wake wa ung’eng’e wafute imani hiyo kwani
Penny ndiye mpango mzima.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati akiwa na 'Penny'.
“Ujue kila mtu huwa ana hisia zake na wengi wamekuwa wakiishi kwa
hisia, nimekuwa nikiambiwa kuwa Wema ana mchango mkubwa katika
uzungumzaji wangu wa Kiingereza jambo ambalo si kweli, aliyenifundisha
lugha hiyo kwa sehemu kubwa ni Penny maana aliniletea hadi mwalimu
ingawa nilikuwa nikimlipa mwenyewe,” alisema Diamond.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment