Mahakama moja huko Los Angeles nchini Marekani imeweka sheria inayowalazimu waigizaji wa filamu za ngono maarufu kama X kuvaa mipira maalum ya kuwakinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa maarufu kama Condom .
Sheria hii ambayo ilianza kama mswada mwaka 2012 inawalazimu waandaaji wa filamu hizi pia kulipia ada maalum ya kupewa kibali cha kufanyia kazi ambacho watalazimika kutafuta kwenye mamlaka husika .
Waandaaji wengi wa filamu za ngono wamelalamikia sheria hii wakidai kuwa inakwenda kinyume na haki zao za msingi japo mahakama imeshikilia uamuzi wake wa kuwalazimisha kuvaa kinga wakati wa upigaji picha za filamu hizi .
Matajiri wa Industry ya filamu za ngono wamedai kuwa wanafahamu fika hatari zilizoko kwenye maambukizi na wanachukua hatua za kupunguza maambukizi haya kwa kujikinga na kuwapima watu wote wanaoshiriki uigizaji wa filamu hizi kabla ya kuingia nao mikataba .
Industry ya filamu za ngono inaingiza fedha nyingi kiasi cha mabilioni ya dola na hofu iliyoko kwa wandaaji wa filamu hizi ni kupungua kwa mauzo yao endapo sheria hii itaanza kutumika .
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment