Sakata
la kusambaa kwa picha hizo zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za
watu maarufu hapa nchini leo limeibuka tena bungeni likiwa na sura mpya
huku baadhiya
wabunge wakitaka kujua serikali inachukua hatua gani juu ya picha
zilizosambaa juzi zinazomuonesha mmoja wa wabunge (jina kapuni) akiwa na
binti mdogo ambazo mwenyewe alikanusha na kudai si za kwake.
Moto
huo ulizidi kuwaka bungeni leo katika kipindi cha maswali na majibu
ambapo Mbunge wa Mchinga (CCM), Mhe. Said Mtanda amehioji serikali
wamechukua hatua
gani dhidi ya vitendo vya uchapaji wa picha zisizozingatia maadili huku akiwataja Wema na Diamond kupiga picha wakiwa chumbani na kuweka kwenye mitandao.
Katika
majibu yake Naibu waziri Habari Utamaduni na Michezo Mheshimu Mkamia,
alijibu kuwa serikali imebaini juu ya matumizi hayo ya picha
Mheshimiwa
Habib Mnyaa aliuliza swali la nyongea kwa wizara ya mawasiliano ya
sayansi na teknolojia ambapo jibu hilo lilijibiwa na waziri wa
mawasiliano
Katika
majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame
Mbarawa anasema “Mhe. Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili
zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu
serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa zikifuatilia Online Content
ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na
kuchukua hatua madhubuti”.
Baada
ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu
juu ya picha za juzi zilizosambaa zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na
binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana
wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe.
Spika kuhusu picha za juzi zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua
zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona
ila tutachukua hatua tutakapobaini zilipotoka.”
Post a Comment