Mambo bado mabaya! Ule ugomvi wa
mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema Bongo, Wema Isaac Sepetu
‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa umechanja mbuga hadi kufika
mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wameingilia kati ili kuumaliza, Risasi Jumatano
linakuhabarisha.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya
mvutano wao wa muda mrefu, wabunge hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo
Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli
wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole.
Ilisemekana kwamba baada ya
kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge hao, hasa wapenda
michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi tatizo hilo haraka,
akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
“Walimwambia Steve kwamba ni kitendo cha
aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana, hiyo inawapunguzia heshima
kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha kushikamana kwa umoja ili kuisogeza
mbele tasnia yao badala ya kulumbana,” kilisema chanzo hicho kikikataa
kutaja majina ya wabunge hao na kutaka aulizwe Steve.
Gazeti hili liliwasiliana na Steve juu
ya ukweli wa madai hayo, ambaye alikubali kuwa ni kweli baadhi ya
wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati ya waigizaji hao maarufu Bongo
kwani nyuma yao kuna vijana wengi wanatamani kuwa kama wao.
Kajala Masanja.
Risasi Jumatano lilizungumza na mbunge
wa Kinondoni Idd Azan ambaye alisema hata yeye atawaunga mkono wabunge
watakaojitolea kuwasuluhisha mastaa hao.
Post a Comment