Wakiongea na ITV katika sehemu za maduka hayo akiwemo Mwenyekiti
wa wafanyabiashara hao wamesema kuwa, hali ambayo imewafanya kugoma ni
kutokana na malalamiko yao kutosikilizwa kwa mda mrefu, pamoja na juhudi
ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi wao jambo ambalo limekuwa ni
kitendawili huku wakiongezewa kodi.
Akizungumza na wafanyabiashara hao mwenyekiti wa kamati ya
ukusanyaji wa kodi wilaya hiyo ya Tabora mjini, ambaye pia ni mkuu wa
wilaya hiyo Bw.Suleimani Kumchaya,amewataka kutokuwa na maamuzi
yanayoathiri jamii bali kufanya makubaliano yanayoleta maendeleo katika
jamii,kuliko kuchukua hatua za maamuzi na za haraka.
Post a Comment