Hali hiyo ambayo haijawahi kutokezea ndani ya baraza hilo ilianza
wakati wajumbe walipokuwa wakianza kuchangia hoja hiyo binafsi ya
mwakilshi wa CUF Mh. Hamad Masoud ambapo mwakishi wa CUF jimbo la
magogoni Mh. Abdillahi Jihad ambaye pia ni waziri alipaonza kumshambulia
wazir wa nchi tawala za mikoa na idara maalum Mh. Haji Omar Kheir
Hapo ndipo sakata hilolilipoanza ambapo naibu waziri amabye ni
CCM Mh. Haji Gavu alipaona kukwaruzana kwamaneno na matusi dhidi ya
mwakilishi wa CUF na kutaka kugeuza ukumbi huo kuwa wa masumbwi.
Pamoja na jitihada za spika Mh. Pandu Ameir Kificho kutaka kuwepo
kwa amani na utaratibu hakiusaidii lolote na fujo hizo zikageuka kwa
wawakilishi wa CCM Mh. Hamza Hassan Juma na mwakilishi wa CUF Mh. Salum
Nassor ambao mnao wataka kuzipiga na kutishiana kwenda nje.
Hili ni tukio la pili kutokea ndani ya mkutano huu wa baraza ambao
wawakilishi wa CUF na CCM kuvutana na kubishana kwa maneno ya matusi na
kejeli.
Post a Comment