Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara-
Korogwe jijini Dar ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa
ikiuliza muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza
kumcharukia bebi wake huyo.
Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mpenzi wake Siwema.
Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:“Wolper ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita maelezo, hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema dizaini kama alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na kila kitu kipo sawa.”
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment