Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WEMA ACHEKELEA KANDAMBILI ZA JOKAT


MBUNIFU wa mavazi na mtangazaji Bongo, Jokate Mwegelo amesababisha shosti yake, Wema Sepetu ‘Madam’ afurahi baada ya kumpelekea zawadi ya kandambili zake za Kidoti pamoja na vipodozi mbalimbali.
Jokate alisema Wema ni miongoni mwa watu ambao anawakubali kutokana na mchango mkubwa katika tasnia ya filamu Bongo, hivyo ameamua kumpelekea zawadi  ya bidhaa zake za Kidoti kuonesha heshima yake.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ akipozi.
“Zawadi zangu niliwapa watu mbalimbali mmoja wapo akiwa ni shoga yangu wa kitambo Wema, hii inaonyesha ni jinsi gani nina mapenzi makubwa kwake,” alisema Jokate. 
Kwa upande wake Wema, alifurahi na kusema amependa zawadi hiyo anamuomba Mungu azidi kumfungulia milango Jokate katika bidhaa zake mbalimbali anazosa-mbaza.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top