MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro imemnyima dhamana Katibu wa Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa katika kesi yake ya
jinai namba 128 ya mwaka 2013 leo.
Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Marry Moyo ambaye
amesema amepokea hati ya kumfutia dhamana Sheikh Ponda kutoka kwa
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kwa mamlaka aliyonayo hivyo yeye
hana mamlaka ya kuikataa hati hiyo.Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Januari 26 na 27, mwaka huu itakaposikilizwa tena.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment