Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Mrithi wa Steven Gerard huyu hapa.



Steven-Gerrard

Baada ya kumshuhudia nahodha wake Steven Gerard akiitumikia klabu hiyo katika msimu huu ambao utakuwa msimu wake wa mwisho baada ya miaka 26 katika klabu hiyo wekundu wa Anfield wataongozwa na mchezaji mwingine .
Klabu ya Liverpool inajiandaa kumtangaza kiungo Jordan Henderson kuwa nahodha wake mpya baada ya kuondoka kwa Steven Gerard mwishoni mwa msimu huu. Henderson alijiunga na Liverpool misimu mitatu iliyopita akitokea Sunderland na baada ya kuanza kwa kasi ya chini amekuja kuwa mchezaji muhimu kwenye klabu hiyo kiasi cha kuaminiwa na kuwa nahodha mpya .
Kocha wa Liverpool Brendan Rogers ameamua kuwa Jordan Henderson atarithi nafasi ya Steven Gerard kama nahodha wa klabu hiyo .
Kocha wa Liverpool Brendan Rogers ameamua kuwa Jordan Henderson atarithi nafasi ya Steven Gerard kama nahodha wa klabu hiyo .

Bado kocha wa Liverpool Brendan Rogers hajaweka wazi uamuzi huu na inatarjiwa kuwa Jordan atatangazwa kushikilia nafasi hiyo muhimu baada ya kumalizika kwa msimu huu .
Pamoja na kuwepo kwa taarifa kuhusu Henderson kukabidhiwa mikoba kama nahodha mpya , bado haijafahamika nani atakuwa nahodha msaidizi kwenye klabu hiyo na inaaminika kuwa huenda kiungo mshambuliaji Raheem Sterling akateuliwa kuwa nahodha msaidizi .
Raheem Sterling anatazamwa kama msaidizi wa Henderson .
Raheem Sterling anatazamwa kama msaidizi wa Henderson .
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top