Katika mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la FA dhidi ya timu ya Yeovil Town kocha Louis Van Gaal aliwashuhudia mabeki wa pembeni Rafael Da Silva na Luke Shaw wakitoka nje huku wakiwa na majeraha yanayohofiwa kuwa ya muda mrefu .
Beki wa kulia raia wa Brazil Rafael Da Silva alipata jeraha baya ambalo linaaminika kuwa la kuvunjika kwa mfupa wa taya baada ya kugongana vichwa na mchezjai wa Yeovil wakati wa kuwania mpira wa juu .
Beki mwingine wa kushoto Luke Shaw aliumia kifundo cha mguu wake baada ya kuwa anacheza kwa maumivu kwa muda mrefu na baada ya kushindwa kuvumilia alilazimika kutoka uwanjani.
Majeraha haya yanafuatia majeraha ambayo yalitokea kwa Ashley Young na Antonio Valencia walioumia kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs huku Marouanne Fellaini akiumia kwenye mazoezi kabla ya mchezo huo .
United bado inaendelea kuwakosa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza kutokana na majeruhi akiwemo kiungo Mholanzi Daley Blind na beki Muargentina Marcos Rojo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment