Msanii wa filamu Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu katika utafiti uliofanyika tangu mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu,imegundulika kwamba Lulu ndie mwigizaji pekee wa kike anaelipwa hela nyingi kuliko waigizaji wa kike wengine hapa bongo.

Jana tarehe 27/01/2015 katika interview aliyofanya Clouds Tv katika kipindi cha Take One kinachoendeshwa na Zamaradi,Lulu aliweza kutaja dau lake endapo mtu atataka kufanya nae kazi.

Lakini kwa Lulu ukihitaji kufanya nae kazi aigize kama main character au muhusika mkuu ni anaanzia millioni kumi na tano "15" hiki ni kiwango cha chini ambacho ukihitaji kumchezesha nje na kampuni yake ya Proin Promotions. Lulu anamiliki kampuni yake mwenyewe inayohusika na utengenezwaji wa filamu zake mwenyewe
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment