Inaelezwa kuwa wakati dereva akiendesha basi hilo ghafla mwanamume mmoja anayedaiwa kuwa ni mzee (mtembea kwa miguu) alikatisha barabarani na kusababisha ajali hiyo.
wakizungumza na mmoja wa askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga aliyeko katika eneo la tukio,ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu yeye siyo msemaji, amesema mwanamume aliyegongwa na gari hilo amefariki dunia papo hapo na kwamba abiria waliokuwa kwenye basi hilo wako salama(hakuna majeruhi wala waliopoteza maisha).
Walioshuhudia tukio hilo wameiambia kuwa dereva wa basi hilo hakuwa katika mwendo kasi ndiyo maana hakujatokea majanga zaidi.
Jeshi la polis limefika katika eneo la tukio na ,Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga Justus kamugishi amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo .na kusema ni mtu moja mtembea kwa miguu alipoteza maisha hapo hapo. Mohab Matukio

USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment