Jumatano ya January 14, kwenye XXL ya Clouds FM Soudy Brown amepiga story na muigizaji Aunty Ezekiel kuhusiana
taarifa kwamba ni mjamzito na ameonekana akinywa pombe, Soudy
alimuuliza kama anafahamu athari za kunywa pombe huku akiwa na ujauzito,
Aunty akasema hazijui na yeye sio mjamzito.
Soudy alimtafuta pia Dk Makongoro kutoka
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye alielezea kuhusu matatizo ambayo
mwanamke anaweza kuyapata iwapo ni mjamzito na anatumia pombe kali,
daktari huyo amesema kuwa mama mjamzito anatengeneza mazingiza ya pombe
kusafiri kutoka kwake kwenda kwa mtoto na kujitunza kwenye sehemu za
ubongo kitendo kinachosababisha mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo kama
mtindio wa Ubongo, Kuzubaa au matatizo ya macho.
Unaweza kuisikiliza U Heard yote hapa.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment