Katika miaka takribani 10 iliyopita 
ulimwengu wa soka umetawaliwa na upinzani wa jadi katika ya wanasoka 
wawili bora kabisa katika kizazi hiki, Mreno Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Lakini pamoja na upinzani walionao 
uwanjani, wanasoka hao wawili wameonyesha kuwa na uhusiano mzuri 
wanapokuwa nje ya uwanja, kwa pamoja wawili hao walionyesha hilo wakati 
walipokuwa Uswisi mwanzoni mwa wiki hii kwenye sherehe za utoaji tuzo ya Ballon d’Or.
Katika kuonyesha hawana uadui, imetolewa video inayomuonyesha Cristiano Ronaldo  akimwambia Lionel Messi kwamba mwanae ambaye ni Cristiano JR ni shabiki wake mkubwa.
Alikaririwa akimwambia: “Mwanangu anakupenda sana, muda wote anaangalia video zako kwenye mtandao wa intaneti“– Cristiano Ronaldo.
Angalia video yenyewe hapo chini 
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
 
 
 
.jpg) 
 
 
 
 
Post a Comment