Ndoa ya Lulu Michael Mwaka 2014 Yabuma, Mwenyewe Asema Hajilaumu Mungu Ndo Kapanga.
SIKILIZA HAPA NA HII NI KASHFA MOJA HIVII
BAADA ya kuwa na malengo ya kuolewa mwaka 2014,
mwigizaji
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kusema imeshindikana lakini
hajilaumu wala hamlaumu mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani
anaamini Mungu ndiye anayewezesha kila kitu.
Akizungumza
na paparazi wetu hivi karibuni, Lulu alisema mwaka 2014 alikuwa na
malengo mengi likiwemo suala la ndoa lakini kwa kuwa Mungu ndiye muweza,
atapanga upya suala hilo na anaamini litakuja kutimia.
“Ndoa
ni mipango ya Mungu, huwezi kulazimisha hata siku moja, sisi wanadamu
huwa tuna mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za
Mungu,” alisema Lulu.
Akizidi
kupiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema kwa mwaka huu na mwakani
hawezi kuweka malengo ya ndoa kwani bado kuna mambo yake hajayaweka sawa
hivyo suala la kuolewa ataliweka hadharani baada ya miaka miwili ijayo.
“Sina
mpango hata kidogo kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka
kupita ndiyo ninaweza kupanga tena suala la ndoa,” alisema Lulu.Alipotakiwa
kumtaja mpenzi aliyenaye kwa sasa, Lulu aligoma kufunguka lakini
akakubali kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe.
“Kwanza
nahitaji mwanaume atakayenielewa kwa kila kitu, pia awe na mapenzi ya
kweli na atakayeniangalia kama Lulu na siyo kama Elizabeth pekee.
Anapaswa kutambua na kusapoti kazi zangu za sanaa,” alisema Lulu.Kuhusu
mikakati yake ya sanaa mwaka huu, Lulu alisema ana mpango wa kuendelea
na masomo huku akiwa pia na ‘project’ kubwa mbili ambazo anatarajia
kuzifanya.
“Nina project kubwa mbili mwaka huu, muda utakapofika kila mmoja atazijua maana nitaziweka wazi,” alisema Lulu.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment