Chelsea ambao wanaongoza ligi leo waliwakaribisha Newcastle United kwenye dimba lao la Stamford Bridge huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao ya kwanza iliyopigwa mwezi uliopita kwenye uwanja wa St James Park.
Magoli mawili ya Diego Costa na Oscar yalitosha kuwapa ushindi Chelsea na kuzidi kuimarisha uongozi wao kwenye msimamo wa ligi.
Wakati huo huo wapinzani Mancheste City walisafiri mpaka kwenye uwanja wa Goodison Park kucheza dhidi ya Everton.
Matokeo ya mchezo huo ni sare ya 1-1, matokeo ambayo yamewafanya Chelsea waendelee kutanua kwenye msimamo wa ligi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment