Msanii
nyota nchini Nigeria Oladapo Daniel Oyebanjo aka D’Banj imeelezwa kuwa
ameingia katika uhusiano wa mapenzi na mrembo kutoka nchini Afrika
Kusini anayejulikana kwa jina la Bonang Matheba.
Msanii wa muziki wa nchini Nigeria D'Banj akiwa na mpenzi wake Queen B
D'Banj
ambaye awali alizama katika dimbwi la mapenzi na wanawake mastaa wa
kinigeria akiwemo muigizaji nyota Genevieve Nnaji na mtoto wa tajiri
Adama Ndimi, tayari ameonesha kuzama kwa mrembo huyo wa nchini Afrika
Kusini.
Imeelezwa kuwa mpenzi wake huyo Bonang Matheba almaarufu kama Queen B ni mtangazaji wa Luninga na Radio, mwanamitindo na balozi wa bidhaa maarufu za urembo nchini humo.
Imeelezwa kuwa mpenzi wake huyo Bonang Matheba almaarufu kama Queen B ni mtangazaji wa Luninga na Radio, mwanamitindo na balozi wa bidhaa maarufu za urembo nchini humo.
Post a Comment