Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Mzuka wa Cindy Sanyu si wa dawa

Msanii wa muziki Cindy Sanyu ambaye macho ya wengi yamekuwa yakimfuatilia kwa sasa, amekanusha kutumia dawa za kuamsha hisia na zile za kulevya ili kumsaidia kuongeza mzuka na ladha katika maonesho yake.
Msasnii wa nchini Uganda Cindy Sanyu
Cindy amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, uwezo wake wa kuandika mashahiri, kuimba pamoja na kutumbuiza jukwaani, ni kipaji, ujuzi na zawadi ambayo ipo ndani yake, huku akisisitiza kuwa hajawahi kutumia dawa za kulevya katika maisha yake.
Kando na tuhuma za matumizi ya Dawa za kulevya, mashabiki wa muziki kwa sasa wanafuatilia kwa karibu kuona ni nini hatma ya mahusiano ya msanii huyu na mpezi wake Ken Muyiisa, hasa baada ya kuonekana kuyumba hivi karibuni.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top