Add caption |
Safari yake ya kutaka kujibadilisha ilianza baada ya kumuona Kim Kadarshian katika Tv shoo inayorushwa na kituo cha E news inayojulikana kama Keep Up with Kardashians miaka michache iliyopita na kuvutiwa na mwanamitindo hiyo maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo macho,mdomo pamoja na sura yake na kutamani kuwa kama yeye.
Akizungumzia sababu za kutaka afanane na staa huyo ambaye ni mke wa rapa Kanye West alifafanua kuwa “huwa navutiwa na midomo ya dada huyu na sehemu mbalimbali za mwili wake,nilicheka sana siku niliposikia watu wananitukanakwa nini nimeamua kufanya upasuaji nakuonekana feki,wanadhani mimi nafanya ili nionekana wa kawaida? kama ingekua hivyo ningewaambia madaktari warudishe pesa zangu,”alisema.
Add caption |
Alisema bado hajamaliza matakwa yake na sasa anafikiria kubadilisha pua yake ifanane na mwanamitindo huyo na endapo ataishiwa fedha za kufanya mabadilio hayo yupo tayari kuazima hata kwa familia yake.
“Muonekano wangu mpya kwa watu unanifanya nijisikie fahari kubwa..napenda watu wanavyotumia muda wao kunitazama,kwa wale wote ambao hawapendi muonekano wangu wajue kuna wengine wanapenda.wajue ndio watu pekee ninaowajali pia”alisema.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment