Kundi la wanawake wanaofanya biashara ya kujiuza nchini Kenya limefanya maandamano kuadhimisha siku ya makahaba duniani jana December 17, lengo lake ni kukomesha dhuluma dhidi yao.
Wanawake hao waliandamana ofisi ya Jaji Mkuu Willy Mutunga wakitaka Serikali kuwapa nafasi ya kuwatambua rasmi na wawe walipa kodi halali kama ilivyo kwa wafanyabishara wengine.
Waandamanaji hao wameishutumu Serikali kwa kuruhusu ukiukwaji wa haki zao za kibinadamu kwa kutokana na kesi ambazo huwa zinawahusu kutochukuliwa hatua za kisheria.
Nilikurekodia sauti na video wakati habari hiyo ikiripotiwa na kituo cha K24, unaweza kubonyeza play kuisikiliza.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment